Benki ya Equity imesaini mkataba na kampuni ya umeme wa jua ya Zola kwa ajili ya kusambaza nishati hiyo kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwainua wateja wao kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Robert Kiboti, alisema lengo la kuingia makubaliano hayo ni kuwawezesha wateja wao kupata umeme jua hususani katika maeneo ya vijijini na mjini.
Alisema mteja atapatiwa mkopo wenye riba nafuu ili aweze kupatiwa nishati ya jua na kuutumia kwa saa 24 bila kulipa chochote.
Kiboti alisema wateja wake wakiwa na umeme itawasaidia katika kuboresha maisha yao kiuchumi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki wa kampuni ya Zola, Johnson Kiwango, alisema walifanya utafiti wao na kubaini kuwapo na tatizo la gharama kubwa katika nishati ya jua.
Alisema lengo la kusaini mkataba huo ni kuwawezesha wananchi kupata sola yenye ubora na kwa gharama nafuu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |