• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Burundi zatakiwa kufanya uratibu kwa karibu, na kulinda mfumo wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-11-12 19:33:17

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China na Burundi zinatakiwa kufanya mawasiliano na uratibu kwa karibu kwenye mambo ya dunia na kikanda na kulinda kithabiti mfumo wa pande nyingi, ili kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizi mbili na nyingine zinazoendelea.

    Bw. Wang ametoa kauli hiyo kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw. Albert Shingiro. Bw. Wang amesema uhusiano kati ya China na Burundi ni mzuri, na nchi hizo mbili zimekuwa zikiaminiana kisiasa kwa kiwango cha juu, na matunda mazuri yamefikiwa kwenye ushirikiano wa kila upande.

    Bw. Wang amesema Burundi imekuwa rafiki wa kila hali wa China, na China itaendelea kuiunga mkono Burundi kulinda mamlaka ya taifa na kupinga uingiliaji kutoka nje. Bw. Wang pia amesema anaamini kuwa Burundi itaendelea kuiunga mkono China kwenye mambo yanayohusu maslahi makuu ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako