• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Somalia ziko tayari kuhimiza uhusiano kati yao katika ngazi mpya

    (GMT+08:00) 2020-11-12 19:33:39

    China imesema iko tayari kushirikiana na Somalia ili kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili kufikia kiwango cha juu zaidi. Bw. Wang amesema hayo kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Somalia Bw. Isse Awad.

    Bw. Wang amekumbusha kuwa China ilikuwa nchi ya kwanza kutambua uhuru wa Somalia, na Somalia ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika Mashariki kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya watu wa China. Pia amesema China na Somalia zimekuwa zinaheshimiana na kutendeana kwa usawa, kwa kuwa nchi zote mbili zimekuwa zikielewana na kuungana mkono kwenye mambo ya maslahi makuu ya taifa.

    Bw. Wang pia amesema Somalia ni rafiki wa kuaminika kwa China, na mwanachama muhimu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, baraza la ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu, na pia zinashirikiana kwenye ujenzi wa ukanda mmoja njia moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako