• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatazamiwa kupata mavuno ya nafaka mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-11-12 20:46:08

    Waziri wa kilimo wa China Bw. Han Changfu kwenye mkutano wa mwaka 2020 wa baraza la ngazi ya juu la maendeleo la China, amesema uzalishaji wa chakula na kilimo wa China umeshinda changamoto ya maambukizi ya virusi vya Corona, mavuno ya nafaka ya China yamehakikishwa na kiasi cha uzalishaji kinatarajiwa kufikia kiwango cha juu zaidi katika historia.

    Bw. Han Changfu amesema mafanikio ya China yanatokana na kutoa kipaumbele katika kuhakikisha usalama wa chakula, na kuongeza uungaji mkono wa kisera na kifedha. Bw. Han Changfu amefahamisha kuwa, tangu mpango wa 15 wa maendeleo ya miaka mitano utekelezwe, China imepata mavuno ya nafaka kwa miaka ya mfululizo, na kiasi cha uzalishaji kimefika zaidi ya kilo bilioni 650 kwa mwaka, kiasi cha wastani cha nafaka kwa kila mtu kimefikia karibu kilo 470, ambacho ni juu kuliko kiwango cha kimataifa cha usalama wa chakula ambacho ni kilo 400 kwa kila mtu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako