• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Africa CDC kutembelea Kenya baada ya maambukizi ya COVID-19 kuongezeka

    (GMT+08:00) 2020-11-13 09:17:21

    Mkurugenzi wa Kituo cha Kukinga na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) John Nkengasong, amesema amepanga kutembelea Kenya ili kujadili hatua za kuongeza mapambano dhidi ya kuenea kwa janga la COVID-19 baada ya maambukizi mapya kupanda kwa asilimia 34.

    Mbali na hapo Nkengasong pia amesema atatembelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC katika juhudi zinazoendelea za kuunga mkono nchi kukabiliana na janga hilo, ambalo limerikodiwa kuongezeka kwa asilimia 8 katika Afrika nzima. Amebainisha kuwa haipaswi kutegea juhudi za kushusha chini mweleko wa maambukizi kwani virusi vina kawaida ya kuonesha dalili kwamba umeshinda na baadae kurudi kwa kasi zaidi. Hivyo amesema wanadhamiria kuchukua hatua za kudhibiti zikiwemo kuvaa barakoa na kuzitaka nchi kuzigharamia.

    Wizara ya Afya ya Kenya ilifanikiwa kuzuia kuenea kwa virusi ilipotekeleza hatua kali za zuio katika nchi nzima, lakini zuio hilo liliondolewa baada ya takwimu za kila siku kuonyesha maambukizi yanapungua, lakini mnamo Oktoba maambukizi hayo yaliongezeka kwa wastani wa asilimia kati ya 15 na 18 kila siku, huku vikiripotiwa vifo zaidi ya 100 karibu kila wiki katika mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako