• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la maambukizi ya COVID-19 nchini Kenya latatiza utekelezaji wa ajenda mageuzi ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2020-11-13 09:17:40

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuongezeka ghafla kwa idadi ya maambukizi ya COVID-19 na vifo nchini Kenya kumeleta kikwazo kipya katika kutekeleza ajenda ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii katika nchi hiyo.

    Akilihutubia taifa kwa njia ya televesheni, rais Kenyatta amesema mbali na kuharibu maisha ya watu ikiwemo kuvuruga utoaji wa huduma muhimu kama afya na elimu, janga hili limepunguza kasi ya maendeleo ya uchumi iliyopatikana mwaka 2019. Hivyo amewataka watu kutorudi nyuma katika juhudi zao za kushinda janga hilo na kuharakisha kuondokana nalo.

    Idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini Kenya jana Alhamis ilifikia 66,723 baada ya watu 919 kugundulika kuwa na ugonjwa huo huku vifo vikipanda hadi 1,203 baada ya wagonjwa 23 kufa kwa virusi hivyo. Novemba 4 Kenya ilitangaza hatua mpya za kuzuia kuenea kwa virusi zikiwemo kuongeza saa za marufuku ya kutoka nje, kusitisha kufungua shule na wafanyakazi wa sekta za umma kufanya kazi wakiwa mbali ya ofisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako