• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama laongeza muda wa mamlaka ya tume ya kulinda Amani huko Abyei

    (GMT+08:00) 2020-11-13 09:18:04

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana liliongeza tena muda wa mamlaka ya Tume ya kulinda amani ya UM huko Abyei eneo linalogombaniwa na Sudan na Sudan Kusini.

    Azimio namba 2550 ambalo limeungwa mkono kwa kauli moja na wajumbe 15 wa baraza hilo, limeamua kupanua marekebisho ya mamlaka ya tume ya kulinda amani kwa miezi sita hadi Mei 15, mwaka 2021. Baraza hilo awali lilirekebisha mamlaka ya Kikosi cha mpito cha UM kinachoshughulikia Usalama huko Abyei UNISFA mnamo Disemba 2011 na kuongeza kazi ya kusaidia mfumo wa pamoja wa Uhakiki na Ufuatiliaji mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini, ambayo ilijipatia uhuru wake Julai 2011.

    Wakati huohuo baraza hilo lilipitisha azimio la kuongeza mamlaka ya Tume ya Kulinda Utulivu ya Umoja wa Matifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA kwa mwaka mmoja mwingine hadi Novemba 15, mwaka 2021. Kupitia azimio lake namba 2552 baraza hilo limeamua kwamba MINUSCA itaendelea kuunda kikosi chenye wanajeshi hadi 11,650 na polisi 2,080 na kuacha dhamira yake ya kufanya idadi hii iwe chini ya hapo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako