• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa nchi za Afrika walaani kampeni ya kuajiri ya kundi la Al-Shabab nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2020-11-13 09:19:06

    Mawaziri wa nchi za Afrika ambazo zinatuma askari wao nchini Somalia walieleza wasiwasi wao kuhusu kampeni ya kuajiri ya kundi la Al-Shabab nchini Somalia.

    Mawaziri ambao kutoka Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia na Djibouti walikutana kukagua hali ya usalama nchini Somalia walitoa taarifa ya pamoja jana wakifuatilia sana juu ya tishio linaloendelea kutoka kwenye kundi hilo na kununua silaha kwao.

    Mkutano huo ulifanyika kufuatia ripoti kuwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabab wameanzisha kampeni ya kuajiri kwa nguvu katika mkoa wa kusini nchini Somalia. Kundi hilo linalodhibiti maeneo mengi ya mikoa ya kusini linaripotiwa kushinikiza viongozi wa vijiji vya mikoa hiyo kuhakikisha vijana wanajiunga na kundi hilo, hali ambayo imesababisha mamia ya vijana kukimbia maeneno hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako