Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alitoa hotuba katika tafrija ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) akisema kuwa China na nchi za Afrika zinahitaji kuimarisha mshikamano na kujenga jumuiya imara yenye mustakabali wa pamoja.
Bw. Wang alitoa mapendekezo manne yakiwemo kuhakikisha uhusiano kati ya China na Afrika unaendana na wakati na kuinuka kwenye kiwango cha juu zaidi, jinsi ya kupata mafanikio zaidi na kuimarisha ushirikiano wa China na Afrika, na jinsi ya kuliwezesha baraza hilo kukabiliana na changamoto na kupata maendeleo kwa njia za uvumbuzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |