• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutuma wataalamu Gambia ni hatua nyingine muhimu ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya

    (GMT+08:00) 2020-11-13 16:59:19

    Kutokana na mwaliko wa serikali ya Gambia, timu ya wataalamu wa matibabu ya China iliwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Banjul jumanne wiki hii, na kuanza kazi ya kuisaidia Gambia kupambana na janga la virusi vya Corona kwa muda wa miezi mitatu.

    Akiwapokea wataalamu hao wa matibabu katika uwanja wa ndege, balozi wa China nchini Gambia Bw. Ma Jianchun, amesema China kutuma timu hiyo ya wataalamu nchini Gambia ni hatua nyingine muhimu ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona na katika sekta ya afya ya umma kwa ujumla, na kumeonesha uungaji mkono thabiti wa China kwa Gambia kwenye mapambano hayo na urafiki wa kindugu kati ya watu wa nchi hizo mbili. Kwa mujibu wa balozi Ma, timu hiyo inaundwa na wataalamu tisa wa taaluma mbalimbali, na baadhi yao waliwahi kwenda mjini Wuhan kupambana na janga hilo.

    Tangu virusi vya Corona vilipuke, China na Gambia zimekuwa zinaungana mkono na kusaidiana katika kukabiliana na janga hilo la pamoja. Baada ya mlipuko wa virusi hivyo kutokea nchini Gambia, China mara nyingi ilitoa misaada ya vifaa tiba na uungaji mkono wa kiufundi kwa Gambia, na timu hiyo iliyotumwa nchini Gambia itakuwa ni timu ya wataalamu wa matibabu ya China iliyotumwa katika nchi za nje kwa muda mrefu zaidi.

    Ushirikiano katika sekta ya afya ukiwa ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya China na Gambia, tangu mwaka 2017 China imerejesha kutuma timu ya madaktari kwenda Gambia, na safari hii timu ya nne ya madaktari kumi iliwasili nchini Gambia pamoja na timu hiyo ya wataalamu ya muda mfupi.

    Balozi Ma amesema, timu ya nne ya madaktari wa China itakaa nchini Gambia kwa mwaka mmoja, na kuisaidia nchi hiyo kupambana na janga la virusi vya Corona na kuinua kiwango cha matibabu nchini humo. Balozi Ma amesema anaamini kuwa wataalamu wa China na timu ya madaktari wa China watatoa msaada mkubwa kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchini Gambia na kufungua ukurasa mpya wa urafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako