• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya taifa ya Tanzania leo inashuka uwanjani mjini Tunis kupambana na Tunisia, inakosa nyota wake watatu.

    (GMT+08:00) 2020-11-13 19:33:58

    Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Simon Msuva amesema wachezaji wamekubaliana kupambana leo kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021. Hii inakuwa ni mechi ya tatu kwa Stars itakayochezwa Uwanja wa Olympique de Rades nchini Tunisia na mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa. Nyota watatu watakosekana ambao ni Thomas Ulimwengu na Adam Adam ambao ni washambuliaji na walipata matatizo kwenye suala la kupata hati za kusafiria na Mbwana Samatta ambaye ni nahodha yeye ni ameshauriwa na madaktari kukaa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10. Msuva amesema kazi ni kubwa na kila mmoja anatambua kwamba wanakwenda kwenye ushindani ila kinachotakiwa kwa sasa ni kuungana, na Watazania waendelee kuwaombea. Kikosi hicho jana kilifanya mazoezi ya mwisho nchini Tunisia kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu. Kikiwa kimecheza mechi mbili kilishinda moja na kupoteza moja kibindoni kina pointi tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako