Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool ametaka a Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kufanya mabadiliko ya ratiba ya ligi hiyo akilalamikia kwamba ugumu wa mpangilio wa sasa ambao una mrundikano wa mechi unaowaumiza wachezaji. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola pia amesema wingi wa mechi zinazopigwa chini ya kipindi kifupi cha muda unachangia idadi kubwa ya majeraha mabaya ambayo yanatishia kulemaza uthabiti wa baadhi ya vikosi. Amesema kwa sasa wachezaji hawapo salama. Wapo katika hatari ya kupata mejeraha yanayotishia taaluma yao, na jambo hili litapunguza viwango vya ushindani na ubora wa ligi. Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pia kubadilishwa kwa muda wa kupigwa kwa baadhi ya mechi kwenye ratiba ya EPL msimu huu ili kuwaondolewa shinikizo wachezaji. Amesema ilikuwa vigumu kucheza dhidi ya Everton ugenini siku tatu pekee baada ya kuvaana na Istanbul Basaksehir kwenye mechi za Klabu Bingwa Ulaya. Kocha wa Everton pia amesema ugumu wa ratiba utaporomosha kiwango cha ligi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |