Mshambuliaji Halid Lwaliwa alitoka benchi na kufunga bao lake la kwanza la kimataifa kwenye uwanja wa nyumbani wa klabu yake wakati Uganda ilipopambana na Sudan kusini kwenye mechi iliyochezwa jumatano jioni dhidi ya Sudan Kusini. Wageni kwa ujumla walilingana nguvu na wenyeji, lakini hawakuwa na bahati na kulazimika kukubaki kichapo hicho. Lakini Lwaliwa, mmoja kati ya wachezaji wawili wenyeji, na mwingine akiwa mbadala wa kipindi cha pili Karim Wantambala, walihakikisha Uganda inadumisha ushindi huo. Kocha wa Cranes Johnny McKinstry alianza na sura mpya ya nne, na ni Joseph Ochaya tu ndiye aliyeanza kati ya waliocheza mechi dhidi ya Malawi. Uganda inaonekana kuwa timu ilivyofanya vizuri kati ya timu za Afrika Mashariki, baada ya Kenya kubanwa mbavu na Comoro, Rwanda kuwabana mbavu Cape Verde na leo Tanzania inajaribu bahati yake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |