• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kutumia sekta ya uvuvi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi

    (GMT+08:00) 2020-11-13 19:39:25

    Serikali ya Uganda imesema inapania kutumia vizuri sekta ya uvuvi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi nchini humo. Waziri wa uvuvi nchini Uganda Bi Hellen Adoa amesema watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa uvuvi haramu haupati nafasi nchini humo. Kauli hiyo ya waziri inakuja wakati ambapo Waganda wengi wamekuwa wakilalamikia uwepo wa askari katika maziwa ya uvuvi nchini humo.Waziri amesema uwepo wa askari hao katika maziwa nchini humo kumesaidia ongezeko la samaki na hata kuchangia pakubwa usafirishaji wa zao hilo nje ya nchi. Benki kuu ya Uganda imesema kati ya Januari na Julai mwaka huu, Uganda imesafirisha nje ya nchi tani elfu 11,402 za samaki za thamani ya dola milioni 72.97. Hata hivyo ameongeza kuwa tani hizo ni chache ikilinganishwa na tani elfu 17,541 za tahamani ya dola za kimarekani milioni 106.53 zilizouzwa kipindi sawa na hicho mwaka jana.Amesema kilichochangia kupungua kwa tani hizo ni msukosuko uliochochewa na janga la corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako