Mamlaka ya Mapato chini Tanzania (TRA) imewasisitizia wafanyabiashara mkoani Mwanza kukata asimilia 10 ya kodi wanazolipa kwa wenye nyumba wanazopanga kwa ajili ya makazi na sehemu za biashara.
Meneja wa TRA mkoani Mwanza Joseph Mtandika amesema kodi ya aina hiyo inakatwa kutoka kwa wenye nyumba kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya mwaka 2004 na kupelekwa TRA.
Mtandika alisema kila mfanyabiashara mwenye TIN namba ana wajibu wa kukata asilimia 10 kila anapomlipa kodi mwenye nyumba na kuiwasilisha kwa TRA.
Alisema wenye nyumba hawana hiari ya kukataa kodi hiyo kwa sababu inakatwa kwa mujibu wa sheria.
Alisema kwa sasa wanakusanya Sh. milioni 700 hadi Sh. bilioni moja kwa mwaka zinazotokana na kodi za wenye nyumba za kupangisha katika jiji la Mwanza.
Alisema kiasi hicho huongezeka au kupungua kwa kutegemea mwezi husika na wameweka msisitizo kuziba mianya yote ya ukwepaji kodi. Kuhusu biashara za magendo kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda kupitia Ziwa Victoria, alisema tatizo hilo limepungua kutokana na mkazo wanaouweka kukabiliana na biashara hizo.
Alisema baada ya nchi za Afrika Mashariki kuweka usawa kwa kodi zinazolipwa, imesaidia kupunguza biashara ya magendo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |