• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Ethiopia ladhibiti mji muhimu katika mkoa wa Tigray

    (GMT+08:00) 2020-11-16 19:41:19

    Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa jeshi la ulinzi la nchi hiyo (ENDF) linadhibiti mji muhimu kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) katika mkoa wa Tigray.

    Taarifa iliyotolewa na kikosi maalum cha dharura kilichoanzishwa na serikali kusimamia operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la TPLF imesema, jeshi la ulinzi la Ethiopia limekomboa mji wa Alamata ulioko Raya ambao ulikuwa ukikaliwa na TPLF.

    Taarifa hiyo imesema, jeshi la nchi hiyo kudhibiti mji wa Alamata ni ishara nyingine kuwa operesheni ya kuhakikisha utawala wa sheria inaendelea kwa umakini huku tahadhari zote zikichukuliwa kuepuka kuleta athari zozote kwa raia.

    Tangu Novemba 4, serikali ya Ethiopia imefanya operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la TPLF, ambalo linatawala mkoa wa Tigray ulioko kaskazini mwa Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako