• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kusaidia kuleta amani ya kudumu katika eneo la Sahel

    (GMT+08:00) 2020-11-17 16:10:11

    Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, Dai Bing amesema, China iko tayari kuendelea kushirikiana na jamii ya kimataifa kuleta amani ya kudumu, utulivu na ustawi katika eneo la Sahel.

    Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Kikosi cha Pamoja cha Kundi la nchi Tano (G5) za Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger, balozi Dai Bing amesema, China inaunga mkono juhudi za kutafuta suluhisho la Kiafrika kwa masuala ya Afrika, na nafasi kubwa zaidi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kwenye masuala ya kikanda.

    Amesema China inatekeleza kivitendo ahadi yake ya msaada wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 45.56 kwa ajili ya operesheni za kulinda usalama na kupambana na ugaidi za kikosi hicho.

    Akizungumzia janga la virusi vya Corona, balozi huyo amesema China imepeleka shehena kadhaa za vifaa vya kupambana na virusi hivyo kwa nchi za kanda hiyo, na pia imechukua hatua ya kubadilishana nazo uzoefu kuhusu janga hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako