• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa wito wa kumaliza mapigano katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-11-17 20:38:14

    Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kumaliza mapigano katika mkoa wa Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, na kuruhusu kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu.

    Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, Umoja huo umeshtushwa na kuongezeka kwa mapigano katika mkoa huo, ikiwemo mashambulizi ya roketi katika mji mkuu wa Eritrea, Asmara, na miji ya Bahir Dar na Gondar katika mkoa wa Amhara nchini Ethiopia.

    Ofisi hiyo imesema, ripoti ambazo bado hazijathibitishwa zimesema, watu wengi wamekimbia makazi yao mkoani Tigray, na idadi ya Waethiopia waliokimbilia Sudan kutafuta hifadhi imefikia 25,300.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako