• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wake na watoto wa waasi wa zamani wa Rwanda warejeshwa katika jamii

    (GMT+08:00) 2020-11-18 16:35:40

    Wake na watoto zaidi ya 1,800 wa waasi wa zamani wa Rwanda waliorejeshwa nchini humo kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwaka jana wameruhusiwa kurejea tena kwenye makazi yao jana baada ya kumaliza kozi ya miezi 11 ye kurejeshwa tena katika jamii.

    Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wake na watoto hao, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Kijamii Ignatienne Nyirarukundo amesema, anatarajia wataishi kwa amani pamoja na wanajamii wengine, wakitetea amani, kuipenda nchi yao na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

    Tangu mwishoni mwa mwaka jana, Wanyarwanda wengi wamerejeshwa nchini mwao kutokea DRC, na wengi wao ni wategemezi wa waasi wa zamani wa Rwanda waliokamatwa na kurejeshwa Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako