Kundi la nne la wakimbizi 79 na watu wanaotafuta hifadhi kutoka Libya limewasili nchini Rwanda jana jioni.
Katibu mkuu wa Wizara ya Usimamizi wa Masuala ya Dharura nchini Rwanda Olivier Kayumba amesema, baada ya kuwasili, wakimbizi hao walipelekwa kwenye hoteli maalum zilizotengwa kwa ajili ya vipimo vya virusi vya Corona, na baada ya kupata matokeo ya vipimo, wahamiaji hao watapelekwa kituo cha dharura cha mpito cha Gashora kilichoko wilaya ya Bugesera.
Kayumba amesema, kuanzia mwaka uliopita, Rwanda imepokea wakimbizi 306 na watu wanaotafuta hifadhi walioondolewa Libya, na 121 kati yao wamepelekwa kwenye nchi nyingine zikiwemo Canada na Sweden.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |