Mazungumzo ya amani ya Afghanistan yamepata maendeleo huko Doha nchini Qatar wakati ambapo timu ya mazungumzo kutoka serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban wamekubaliana juu ya ajenda muhimu.
Pande mbili zimekubaliana kujumuisha idhini ya Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani wa Afghanistan, ahadi za timu za mazungumzo, matakwa ya Wafghanistan pamoja na makubaliano ya amani kati ya Marekani na Taliban kama msingi wa masuala makuu ya kiutaratibu na msingi wa mazungumzo.
Mazungumzo hayo ya amani yamekuwa yakiendelea huko Doha tangu mapema Septemba mwaka huu, ili kupata ufumbuzi wa amani kwenye mgogoro wa muda mrefu wa Afghanistan. Tofauti kati ya pande mbili juu ya utaratibu, sheria na kanuni vilikuwa vikwazo vikubwa vya mazungumzo. Ripoti hiyo imekuja wakati ambapo mkutano wa kimataifa juu ya Afghanistan unatarajiwa kufanyika huko Geneva, Uswizi leo Jumatatu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |