Jumla ya watu 516 wanaodaiwa kujihusisha na shughuli za ugaidi katika mkoa wa Cabo Delgado uliopo kaskazini mwa Msumbiji ambao wanashikiliwa nchini Tanzania watarejeshwa Msumbiji kwenda kushtakiwa.
Watu hao wanaoshukiwa kuwa ni magaidi waliingia Tanzania wakitarajia kukimbia kukamatwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Msumbiji lakini wakaishia kushikiliwa na mamlaka za Tanzania. Kamanda mkuu wa Polisi ya Jamhuri ya Msumbiji Bernardino Rafael amesema mamlaka za polisi za nchi mbili zimesaini makubaliano ya maelewano wikiendi iliyopita huko Tanzania, ya kuwarejesha watu hao wanaoshikiliwa, wakiwemo washukiwa wa ugaidi na watu walioshirikiana nao. Rafael amebainisha kuwa watu hao waliozuiwa wanatoka Msumbiji, Tanzania, Somalia, Uganda, DRC, Rwanda na Burundi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |