Kutokana na mwaliko wa mwanamfalme Salman bin Hamad Al Khalifa, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu leo amesema atatembelea Bahrain hivi karibuni.
Kwenye taarifa yake kwa njia ya video, Netanyahu amesema yeye na mwanamfalme waliongea kwa simu Jumatatu kuhusu njia za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili. Amesema hayo ni mazungumzo ya pili na kuyaelezea kama ni ya kirafiki. Septemba 15, Israel na Bahrain zilisaini makubaliano ya kufanya uhusiano wao urejee katika hali ya kawaida ambayo yalipatanishwa na Marekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |