Suzhou ni moja kati ya vituo vitatu vikubwa vya uzalishaji wa vitambaa vya hariri nchini China, na inasifiwa kuwa ni "chimbuko la vitambaa vya hariri". Kuna watu wanaosema kuwa Suzhou ni kama mwanamke mwenye sura nzuri wa mashariki, vitambaa vya hariri ni kama nguo yake ya kuvutia zaidi; Suzhou ni pepo ya duniani, vitambaa vya hariri ni kama mawingu ya alfajiri yenye rangi za kupendeza peponi. Kama tunasema, vitambaa vya hariri na vyombo vya kauri ni alama mbili za utambulisho wa taifa katika historia ya China, basi vitambaa vya hariri ni kadi moja ya jina lenye maneno ya kidhahabu ya Suzhou.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |