Siku ya wapendano inayojulikana kwa kimombo Valentine's day huwa ni February 14 ya kila mwaka, na mwaka huu kama kawaida inasubiriwa kwa hamu na wale walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, kuliko yale ya kifamilia.
Kuanzia mwanzoni mwa mwaka wa 2000 mpaka leo siku hii imekuwa na shamrashamra sana katika nchi mbalimbali hasa za Afrika ingawa sio rasmi, yote hiyo ni kutokana na tamaduni za kimagharibi kuingia sana katika bara hilo na kuigwa hasa na watu wa kizazi kipya,kutokana na ukuaji wa teknolojia hasa internet,simu za mkononi,TV hata vituo vya Radio ambavyo vimeingiza kwa kasi kubwa tamaduni za kimagharibi katika nchi hizo.
Siku hiyo inapambwa zaidi na mavazi ya rangi nyekundu na maua mekundu ya waridi, kila kona na kila utakaekutana nae siku hiyo hasa vijana basi atakuwa amevaa nguo nyekundu au hata kuwa na kitu kidogo tu chenye rangi nyekundu ambayo wengi wanadai kuwa ni rangi ya upendo.
Nchini China ni tofauti kidogo na nchi nyingine, siku hii haina nafasi sana kwao kwa maana wao Wachina, wanajali sana tamaduni zao ingawa hivi sasa baadhi ya vijana wa kizazi hiki cha sasa wanaihusudu siku hiyo.
Wachina wao hupeana zawadi kama apple tu na vitu vingine,kwa kuwa siku hii haina maana kwao, wanaamini mapenzi ama upendo hautengewi siku upo kwa maisha yote.
niliwahi kuongea na kijana mmoja mchina kuhusu Valentine day moja kwa moja alinipa jibu rahisi sana kuwa kwake haina umuhimu na kuongeza kuwa kupendana hakuna siku maalum.Akaongeza kuwa kumpa
zawadi mpenzi wako hakuna siku maalum pia.
Mwaka jana 2011 wakati nipo mji wa Wuhan, Valentine's day ilikuwa ya kawaida sana ingawa baadhi ya wazawa yaani wachina walipeana zawadi moja na nyingine tena wale ambao wanaiga tamaduni za kimagharibi hasa vijana wachache.
Kijana mmoja anaeitwa Suleimani toka nchini Tanzania anasema kwa yeye anavyojua siku hiyo haina maana hata kidogo
Kwake mara nyigi siku hiyo wengi huenda katika kumbi za usiku za starehe na kufanya matendo maovu ambayo ni kinyume na tamaduni zetu
Siku hii ya Valentine's day ilibuniwa na kiongozi mmoja wa dini ya kikristo miaka kadhaa iliyopita aliyeitwa Valentino ikiwa na maana upendo zaidi katika maisha ya mwanadamu na familia yake ila jinsi miaka inavyokwenda siku hii imekuwa ikiadhimishwa tofauti na malengo yake.
Cha kushangaza zaidi kuwa pamoja na siku hiyo kuanzishwa na kiongozi wa dini hivi sasa wakuu mbali mbali wa dini wanaipiga vita siku hii baada ya watu kuiadhimisha tofauti na malengo sahihi ya siku hiyo.
Jamii nyingi zikiwemo za kiafrika zinaipinga siku hii kwa kuwa si utamaduni wa Kiafrika na kuwa inapotosha vijana wengi sana. Ninaunga mkono sana wananchi wa China kutoipa nafasi siku hii ambayo inapotosha tamaduni zetu ambazo hivi sasa tunapigana kuziimarisha kutokana kuingiliwa na tamaduni za kimagharibi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |