• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari wanafunzi kufungua Cliniki za dawa asili za kichina katika nchi zao za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-28 18:03:18

    Wanafunzi wawili wa kike kutoka katika nchi za Afrika wanaosomea jinsi ya kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa kutumia dawa asili za kichina wamesema lengo la kusoma masomo hayo ni kufungua Kliniki za matibabu hayo nchini mwao.

    Wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini dawa hizo ni tiba sahihi kwa magonjwa mengi .

    Wanafunzi hao pekee wanaotokea Afrika Vannesa Njitack (25) kutoka nchini Cameroun na Badra Said Ali (26) kutoka nchini Commoro ni wanafunzi pekee wanaosoma masomo hayo katika Chuo Kikuu cha dawa Asilia za Kichina cha Nanjing.

    Wakizungumzia sababu za kujiunga na masomo hayo na siyo udaktari wa kawaida kutoka nchi za Magharibi kwa namna tofauti walionekana kuamini matibabu ya dawa hizo ndiyo sababu ili kuwasaidia wananchi wa nchi zao.

    Njitack ambaye yuko mwaka wa kwanza katika masomo hayo ya miaka mitano anaeleza kuwa baada ya kuona kuna watu nchini mwake wanatumia dawa hizo na kupona magonjwa mbalimbali alitaka kujua nini ni siri ya dawa hizo.

    Alisema dawa hizo ni tofauti na zile za asili kutoka afrika kwani zipo unazoambiwa zinatibu ugonjwa Fulani lakini ukitumia huponi lakini za asili za kichina zimefanyiwa utafiti na kuunganisha vitu vya asili ambavyo mtu akitumia anapona kabisa.

    "Dawa hizi pia zipo za kuchanganywa kwenye supu au chai kama una matatizo yanapona kabisa mfano mzuri ni kwa watu wenye matatizo ya moyo au kisukari"alisisitiza na kueleza kuwa akimaliza chuo ataangalia namna ya kutoa matibabu hayo nchini mwake.

    Lakini kwa Ali ambaye mwaka wa tatu kati ya miaka mitano ya kusoma matibabu hayo anasema mikakati yake ni kufungua Kliniki yake ya dawa asili za kichina.

    Anasema kuna baadhi ya vifaa vinaweza kupatikana kirahisi lakini kwa madawa mengine anahakikisha anakuwa na marafiki watakaomsaidia kupata dawa hizo na kutoa matibabu yake kwa urahisi.

    "Mjomba wangu alisomea matibabu haya na nikamshuhudia akimpatia matibabu ndugu yangu aliyekuwa na matatizo ya uzazi na baada ya muda alipata motto hivyo nikaona vema kuja zusoma na kuzijua kwa undani ili kusaidia wananchi wa nchi yangu"alisema

    Chuo hicho chenye miaka 36 tangu kuanzishwa kutoa matibabu ya asili ya kichina kwa sasa ina wanafunzi 20,000 na kati yao 1500 ni kutoka mataifa mengine duniani wakiwemo hao wawili kutoka Afrika huku mwaka jana wakimaliza mafunzo wanafunzi wane toka Afrika na kurudi kutoa matibabu katika nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako