• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda cha viatu China kutoa ajira 100,000 Afrika

    (GMT+08:00) 2017-04-21 08:38:01
    Na Theopista Nsanzugwanko, Guangdong, China

    KIWANDA kikubwa cha kuzalisha viatu vya kike nchini China cha Huajian Footwear Manufacturing kimeeleza nia kuwekeza zaidi katika nchi za Afrika na kutoa nafasi za ajira 100,000.

    Pia kiwanda hicho pia kimesema kinatarajia kuwapatia mafunzo ya utengenezaji wa viatu hivyo vya kisasa wananchi wa Afrika zaidi ya 2,000 watakaopatiwa mafunzo nchini China.

    Rais wa Kampuni ya Huajian Group, Huarong Zhang alisema hayo wakati waandishi wa habari kutoka nchi 27 za Afrika walipotembelea Kiwanda hicho kilichopo katika mji wa Dongguan, Guangdong kuwa nia yake ni kuajili waafrika hao katika miaka 20 ijayo.

    Alisema ajira hizo kwa wananchi kuoka nchi zenye uchumi wa kati ,zinazojali ubora na uaminifu katika kujiletea maendeleo huku zikiwa na utulivu wa kisiasa,usalama wa watu na vitu.

    Zhang alisema nchini tayari wameanza kuwekeza nchini Ethiopia katika kiwanda chake cha Huajian International light industry City ambacho kimeajili wafanyakazi zaidi ya 6,000 huku akiwa na mpango wa kukipanua zaidi kiwanda hizo ifikapo mwaka 2020 .

    Alisema katika kiwanda hicho huwalipa mshahara dola za marekani 75 hadi 95 huku wengine wakipatiwa mpaka dola 500 hadi 1,000 kwa ngazi za juu wakati kiwango cha chini cha mshahara kwa sekta hiyo kilichopangwa na serikali ya Ethiopia ni dola 15 hadi 20.

    Alisema rasilimali kwa kiwanda chake cha nchini Ethiopia wanapata kutoka nchini humo kwa asilimia 50 huku asilimia 20 ikitoka nchini China na asilimia 30 nchi nyingine za Afrika.

    Zhang alisema kampuni hiyo inayozalisha pea za viatu zaidi ya milioni 20 katika viwanda hivyo viwili na kuuzwa katika soko lake kubwa katika nchi za Marekani na Ulaya ambapo wana wateja wao wanaotoa oda kwa nembo maalum au watu mashuhuri.

    "Katika viwanda hivi vyote viwili tunatengeneza viatu vya kike ambavyo hatuuzi katika nchi hizi za China na Ethiopia lakini tunapeleka katika masoko ya nchi za ulaya,na tumekuwa tukipata wateja wengi kila wakati" alisema.

    Alisema mauzo ya jumla ni dola za marekani milioni 300 na kupata faida ya asilimia tano yake na wamekuwa wakitengeneza viatu vya kike kutokana na oda wanazopata toka kwa wateja wao.

    Alisema mpaka sasa zaidi ya waafrika 150 wameishapatiwa mafunzo katika kampuni hiyo na sasa wapo 50 wakiendelea na mafunzo huku wakiwa na mikakati ya kuajili wafanyakazi 1000 hadi 2,000 katika nchi za Afrika na kuwapatia mafunzo nchini China ili waweze kufahamu ufanyaji kazi wa kampuni hiyo.

    Alisema kwa waafrika watakaoenda kupata mafunzo nchini humo wataelezwa jinsi wanavyofanya kazi kwa ubora unaotakiwa na masuala mengine yanayohusu utengenezaji wa viatu vyenye ubora katika viwanda vyao.

    Akizungumzia sababu za kuwekeza nchini Ethiopia anaeleza kuwa ilitokana na ziara ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Meles Zenaw nchini China na kumhamasisha kwenda kuwekeza nchini humo na baada ya kuamua kuwekeza amepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa serikali hiyo na kutaka nchi nyingine za Afrika kufungua milango ya uwekezaji ili kujipatia maendeleo.

    Kampuni ya Huajian ilianza mwaka 1984 katika mji wa Nanchang nchini China kukiwa na wafanyakazi 18 na mashine tatu lakini baadaye mwaka 1996 ilihamia Dongguan na kuanzisha kampuni iliyokuwa na wafanyakazi 600 na kuzalisha pea za viatu milioni moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako