Katika mfululizo wa mipango ya 13 ya China ndani ya miaka mitano (2016-2020), serikali ya China imeweka bayana kwamba inategemea uvumbuzi kuongeza ukuaji wake. Kwa mujibu wa utawala huo wenye makao makuu Beijing, hii itakuza nguvu mpya katika utekelezaji wake wa mikakati ya maendeleo yanayotokana na msukumo wa uvumbuzi.
Makampuni yote ya Kichina, kubwa na ndogo, kama nilivyogundua, kwa muda mrefu yamevutiwa na wito huu na wameukumbatia. Mojawapo wa kampuni hizi ni ile ya teknologia na mawasiliano ya Huawei. Kampuni hiyo inasema kupanda kwa sifa yake na kuinuka kwa umaarufu wake duniani umetokana na uaminifu wake kwa sayansi na teknolojia. Hivi sasa, ni vigumu kwa yeyote kukataa kwamba vifaa vya Huawei hazipo kati ya zile bora zaidi ulimwenguni kwa masuala ya ubora.
"Sisi tunaongezeka kwa kasi katika masuala ya kiasi cha mauzo ya yeyote ya makampuni ya Kazindata au smartphone. Watu wengi duniani kote wanazidi kutambua thamani ya vifaa vya Huawei. Sisi tumesafirisha nje milioni 139 ya simu hizi mwaka jana." Joe Kelly ambaye ni makamu wa rais wa masuala ya kimataifa kuhusu masuala ya vyombo vya habari katika kampuni hiyo alisema.
Utafiti na Maendeleo
Kampuni hiyo inasema utafiti na maendeleo ni uti wa mgongo wa shughuli zake. Hadi sasa imewekeza katika vituo vya R&D 16 kote duniani na inapanga kuongeza vituo hivi. Kwa miaka mingi, uwekezaji wake katika sekta ya ubunifu imeongezeka marudufu.
Jaribio hili kulingana na kampuni hiyo imefanya mtengenezaji huyo wa simu kuhesabiwa miongoni mwa viongozi wa dunia katika sekta hiyo. Kwa sababu hii kampuni ya Huawei imeendelea kuwekeza rasilimali nyingi kwa utafiti na maendeleo na hautakoma kufanya hivyo hivi karibuni.
"Kile kinachotutofautisha na washindani wetu ni ahadi yetu ya Utafiti na Maendeleo. R&D umeletea Huawei ushindani zaidi, kusukuma sekta mbele na kuendesha mabadiliko ya teknolojia." Alisema Kelly.
Kwa kweli, kati ya nguvu kazi ya 170,000, kumbukumbu katika kampuni hiyo yenye mizizi yake mjini Shenzhen, mkoani Guangdong, ulibaini kuwa 100,000 hasa walioajiriwa wanajukumu la kufanya kazi katika vituo vyake vya utafiti na ugunduzi.
"Jinsi mapato yetu yanaendelea kukua, kiasi cha fedha ambacho sisi tunawekeza kwa Utafiti na Maendeleo inaongezeka pia. R&D imetusaidia kuendelea kwa haraka. Ni mwaka wa 2012 pekee wakati sisi tulianza biashara ya smartphones ikilinganishwa na washindani wetu." Kelly alisema
Si jambo la kushangaza kwamba kampuni hiyo ilitajwa kati ya makampuni 100 wavumbuzi duniani katika mwaka wa 2014 na Thompsons Reuters. Kampuni hiyo inasema hii inahalalisha idadi kubwa ya mapato inayorejeshwa kwenye mpango wa utafiti na ubunifu.
"Tuna sera katika kampuni ya kuwekeza asilimia kumi (10%) ya kiwango cha chini cha mapato yetu tena kwenye R&D kila mwaka. Tumekuwa na sera hii tangu mwanzo. Hiyo ndiyo sababu kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa." Alibainisha bwana Kelly.
Ndani ya mwongo mmoja uliopita, kampuni hiyo inasema utafiti na maendeleo yake umesaidia katika uzalishaji wa vifaa mpya, mitandao mpya, klabu ya kompyuta mpya, na njia mpya ya kufanya mambo.
Mwanzo usioridhirisha
Kampuni hii ni mfano halisi wa hadithi ya kutoka chini kufikia neema. Ren Zhengfei, mhandisi wa zamani katika jeshi la China PLA, alianzisha Huawei mwaka wa 1987. Wakati huo, Huawei iliingia soko la teknologia kama mtengenezaji mnyenyekevu wa swichi ya simu.
Hatua hii ilitokana na shinikizo kutoka serikali ya China wakati huo kutafuta maendeleo katika miundombinu ya mawasiliano ya simu iliyokuwa duni nchini humo.
Wakati makundi mengine ya utafiti ya Kichina yalitafuta ubia na ushirikiano na makampuni imara ya kigeni, bwana Ren alichukua barabara isiyofahamika. Yeye alilenga kuzalisha swichi hiyo kupitia kugeuza-uhandisi au reverse-engineering, kwa kurekebisha kile kilichosafirishwa kutoka mataifa ya nje na kuhainisha na hali ya ndani kwa njia ya utafiti.
Hii baadaye ilionekana kuwa mradi uliofanikiwa kutokana na kwamba yeye hatimaye alisaidia kujenga mawasiliano ya simu na teknolojia ya Kichina ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ndoto. Tangu wakati huo, Huawei imenawiri na kuwa kiongozi wa kimataifa katika mitandao ya mawasiliano ya simu.
Uwazi wa ushirikiano
Lakini inaonekana kampuni hii, yenye makao yake makuu katika mji wa Shenzhen, ilichukua njia kadhaa ili kusaidia ukuaji wake haraka katika mazingira ya teknologia ambayo milele inabadilika na kuwa na ushindani. Mbali na ubunifu, kampuni hiyo inasema imekubali mteja kuwa nguzo yake. Hii kwa kiasi kikubwa ingeafikiwa kupitia njia ya kujitolea kwa uwekezaji mkubwa na kuendelea pamoja na dhamira ya mfumo wa thamani inayotokana na kushiriki nguvu kazi ya kimataifa.
"Sauti yenye nguvu zaidi katika yote ni ile ya wateja wetu. Sisi tunasikiliza kwa makini mahitaji yao. Huawei inanakili matatizo yao na wahandisi wetu wanatafuta njia za kuyatatua." Kelly ambaye asili yake ni Uingereza anasema.
Huawei inabainisha kuwa ukuaji wake endelevu imeimarishwa na sera yake ya ushirikiano wa uwazi kwa kushiriki mafanikio na washirika wa kimataifa.
Kwa sasa, kampuni hiyo imeshirikiana na vyuo vikuu na watafiti tajika duniani katika ulingo wa uvumbuzi huku ikiorodhesha msaada wa wauzaji maarufu duniani kama vile Foxconn, IBM, Oracle na Qualcomm miongoni mwa wengine.
Ubora wa Bidhaa
Kufikia sasa Huawei inasema haitalegeza kamba kwa swala la ubora wa vifaa vyake kwa ajili ya wingi wa mauzo.
"Huawei kamwe hatutaendea bei ya chini, gharama ya chini au ubora wa chini kwani itadhoofisha faida ya kimkakati ambayo tumejenga katika miongo miwili iliyopita." Kelly alielezea.
Kwa kupiga darubini siku za baadaye, kampuni ya Huawei inasema itaendelea kuwekeza sana katika R&D baada ya kutenga bilioni 10-20 Dola za Marekani kila mwaka kwa ajili ya mpango huu.
Siku hizo za baadaye kwa bahati nzuri Afrika yaonekana kuwa na nafasi. Kampuni hiyo ilibainisha kuwa macho yake imeangazia barani humo na kwamba inafuatilia kwa sana mambo yanavyoendelea Afrika kwani inatambua kuibuka kwa Afrika kama soko yenye nguvu na muhimu sana. Hata ingawa hakuna vituo vya R&D katika Afrika kwa sasa, Kelly anasema hii itabadilika hivi karibuni.
"Sisi ni tunaangalia ni wapi tutaweka shughuli zetu katika Afrika. Inaweza kuwa katika Utafiti na Maendeleo, huenda katika vifaa, huenda ikawa kitu kingine." Alisema.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |