• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Ukanda Mmoja na Njia Moja" fursa kwa Afrika kuunganishwa na nchi nyingine duniani kwa Miundombinu

    (GMT+08:00) 2017-05-12 15:40:24

     

    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    NCHI za Afrika zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi ya miundombinu jambo lililofanya kuwa ngumu kwa kuunganisha bara hilo kutoka nchi moja hadi nyingine.

    Kutokana na changamoto hiyo, hata mzunguko wa bidhaa katika nchi hizo umefanya kuwa mgumu na nyakati nyingine kusababisha kuwa na gharama kubwa huku kukiwa na uwezekano mdogo wa kutoa bidhaa sehemu moja ya dunia kwenda nyingine kwa ajili ya kukuza maendeleo na uchumi wa bara hilo na nchi moja moja.

    Lakini China kupitia pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ulioasisiwa na Rais wake Xi Jinping mwaka 2013 wameshirikisha nchi za Afrika kwa lengo la kufungua milango na kuunganisha nchi za Afrika na nchi nyingine duniani zaidi ya 60.

    Ukanda Mmoja na Njia Moja ni Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne 21 na kuunganisha miundombinu, kwa lengo la kujenga njia tatu zinazounganisha China na bahari ya Baltic, ghuba ya Uajemi na bahari ya Hindi.

    Mkutano wa kilele wa baraza la kimataifa la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utafanyika jumapili wiki hii yaani Mei 14 hadi 15 mwaka huu mjini hapa na kuhudhuriwa na wakuu wa nchi zaidi ya 28 huku Afrika akihudhuria Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn pamoja na mawaziri na watendaji mbalimbali.

    Macho na masikio ya watu duniani yameelekezwa katika mkutano huo utakaohudhuriwa na Rais wa China ambaye ndiyo mwanzilishi wa pendekezo hilo katika kufungua milango ya nchi hiyo na nyingine duniani kufahamu mafanikio na matarajio yake.

    Pendekezo hilo limekuwa msukumo muhimu wa kuhimiza maendeleo ya jumuiya ya kimataifa,huku likienda sambamba na mipango ya Afrika ya kuunganisha nchi zote kwa barabara, reli na ndege ili ziweze kufanya biashara pamoja.

    Mkakati huo umetoa fursa kwa nchi ya China na zilizo Afrika kufanya kazi pamoja ajili ya maendeleo kwani licha ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya pendekezo hilolakini kwa Afrika waliongezewa nyingine Dola za Marekani milioni 60 katika mkutano wa Ushirikiano kwa nchi za Afrika na China (FOCAC)uliofanyika mwaka 2015.

    Ujenzi wa Miundombinu ikiwa ni lengo la kwanza la pendekezo hilo,kwa ajili ya kuunganisha nchi zote 54 za Afrika kwa kupitia miradi mbalimbali ya usafirishaji ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa,Viwanja vya Ndege,Reli kwa ajili ya Trani za Mwendo kasina na Bandari.

    Pendekezo hilo limejikita katika masuala mbalimbali lakini kubwa ikiwa ni maendeleo ya miundombinu kuunganisha nchi za ukanda mmoja na miradi ya maingiliano ya nchi hivyo kuleta maendeleo na bara hilo pamoja na kuhamisha viwanda kutoka China mpaka Afrika hivyo kurahisisha usafirishaji wa bidhaa.

    Katika dola za marekani bilioni 60 ikiwa ni mkopo kwa afrika iliyotolewa katika mkutano wa FOCAC huko Johannesburg, zaidi ya nusu zitatumika katika ujenzi wa miundombinu.

    Pendekezo hilo limeanza kuonesha mafanikio kwa nchi za Afrika katika kujenga miradi ya usafirishaji na miundombinu hususan kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuanza na mradi mkubwa wa reli nchini Kenya na Djibouti ambapo miradi ya miundombinu inafanywa na kampuni toka China na kufadhiliwa kwa mkopo na Benki ya Exim China.

    Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) nchini Kenya unakadiliwa kugharimu dola za marekani bilioni 3.8 inajengwa kutoka Mombasa hadi Nairobi na unajengwa na Kampuni ya China na unatarajia kukamilika baadaye mwaka huu, huku benki ya Exim ikigharamia asilimia 90 ya Ujenzi na serikali ya Kenya wakitoa asilimia 10.

    Baada ya kukamilika reli hiyo inatarajia kuunganisha eneo la Mombasa Uganda, Rwanda na Sudan Kusini,jambo litakalosaidia kuongeza maendeleo ya kiuchumi kwa nchi zote zitakazokuwa zimeunganishwa.

    China kupitia mkakati huo wanashiriki katika ujenzi wa bandari ya Lamu nchini Kenya inayojengwa na Kampuni ya China Communications Construction iliyowekeza dola za marekani milioni 480 katika ujenzi wak.

    Mradi huo wa bandari mpya ya Lamu utakapokamilika sehemu ya bandari hiyo katika Sudan Kusini na Ethiopia inatarajia kunufaisha Afrika nzima.

    Djibouti, nchi yenye idadi ndogo ya watu nayo imeingia mkataba na China kutumia bandari yake kama kitovu cha biashara pamoja na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege,pamoja na Reli ya kisasa kati ya Ethiopia-Djibouti yenye urefu wa kilometa 752.7 uwezeshaji wa dola za marekani bilioni nne huku ukijengwa na kampuni za Kichina kutokana na kuwa Djibouti ni njia muhimu ya usafirishaji nchini Ethiopia na kitivyo cha biashara kuingiza na kuuza bidhaa kwenda au kutoka nchi za Asia, Ulaya na nchi zote za Afrika .

    Ethiopia inatarajia kujenga mtandao wa reli wenye kilometa 5,000 itakayounganisha nchi hiyo na Kenya, Sudan na Sudan kusini, Djibouti ni mtandao mwingine tarajiwa wa usafirishaji Afrika itakayounganisha bahari ya Red Sea na Atlantic.

    Nchi nyingine katika bara hilo iliyonufaika na mkakati huo ni mradi wa ujenzi wa Bandari ya Kisasa ya Bagamoyo nchini Tanzania,pamoja na ukarabati wa Reli ya TAZARA ambayo ni alama mahususi ya ushirikiano wa nchi ya Tanzania na China iliyojengwa miaka ya 70 ambayo itasaidia kuunganisha mawasiliano na nchi nyingine Afrika.

    Majadiliano ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo yalianza mwaka 2016 na kampuni mbalimbali na ujenzi wake ukikamilika itakuwa moja ya bandari kubwa Afrika inayounganishwa na mtandao wa reli na barabara na kuunganisha nchi nyingine za Afrika Mashariki.

    Nchi nyingine za Afrika zinazoonesha shauku ya kujumuishwa katika pendekezo hilo ni Mauritania, Guinea na Togo.

    Katika nchi za Afrika ya kati nchi Cameroon ni njia ya Afrika Magharibi na kati katika kuunganisha miundombinu ya usafirishaji hasa kwa kutumia bandari yenye kina kirefu cha maji ya Kribi iliyojengwa na kampuni ya Kichina huku ikitarajia kuunganishwa na nchi nyingine katika Afrika Magharibi kama ibreville, Gabon; Tema, Ghana na Dakar, Senegal.

    Nchi nyingine kama Nigeria, inatafuta mkopo katika kujenga reli kutoka Calabar mpaka Lagos unaojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction kwa dola za marekani bilioni 12 katika mradiitakayofikia miji yote 10 iliyo Pwani ya Nigeria.

    Pendekezo hilo la China katika ujenzi wa miundombinu kwa China na maeneo ya Afrika imefungua mlango wa maunganisho kwa nchi zote katika nchi za Afrika na nyingine duniani baada ya kukamilika kwa miradi mingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako