Nchi nyingi katika bara la Afrika zimekuwa zikikabiliwa na ukosefuwa nishati ya umeme ya uhakika hivyo kupoteza kupata wawekezajikatika sekta mbalimbali hasa viwanda huku wawekezaji wengine wakitishia kuondoka kwa madai ya kukwamisha uzalishaji na kuongeza gharama.
Inaelezwa kuwa katika kutatua matatizo ya umeme barani Afrika kutahitaji matumizi ya nishati ya ufanisi mkubwa na nchi kutumiarasilimali walizonazo kuhakikisha wanajiletea maendeleo. Dongfang Electric Cooperation (DEC) ni kampuni kubwa nchini China ya kuzalisha umeme na kuuza vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuzalisha au kusambaza umeme kwa kutumia nishati mbalimbali.
Kampuni hiyo iliyopo katika mji wa Chengdu katika jimbo la Sichuan ilianzishwa mwaka 1958 na kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Jua, Upepo, Nyuklia, Makaa ya mawe, Maji na nyinginezo. Kampuni hiyo ni ni moja ya uti wa mgongo katika biashara ya kuzalisha nishati mbalimbali nchini China, DEC imekuwa na mfumo mpana katika sekta ya viwanda, utafiti na maendeleo ya teknolojia. Katika kuhakikisha wanakabiliana na Changamoto kubwa ya nishati ya umeme katika bara la Afrika, Kampuni hiyo inaalika Serikali zanchi hizo kuwatumia katika kukabiliana na changamoto hiyo kubwa kwani wanazalisha kwa ubia kati ya serikali hizo na China.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya DEC, Hu Weidong anaweka wazikuwa kampuni hiyo yenye uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika uzalishaji wa nishati mbalimbali za umeme na kuzingatia utunzaji wa Mazingira imekuwa na mafanikio makubwa. Anasema katika nchi mbalimbali ambazo wameishaanza kutoa huduma duniani wamefanikiwa kuzalisha umeme wa nishati za Jua, mvuke, gesi asilimia, maji, Nyuklia, Makaa ya mawe na nyinginezoambazo zinapatikana maeneo husika. Anasema DEC ipo tayari kufanya kazi na nhi yeyote ya Afrika kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya pande hizo mbili hivyo ikiwa nchi hizo zitaalika kampuni hiyo itahakikisha wanamaliza changamoto hiyo. "Teknolojia mbalimbali katika kuzalisha umeme ni changamoto kubwa kwa nchi za Afrika licha ya kuwa na nishati mbalimbali zinazoweza kupata nishati hiyo"anasema.Anaeleza kuwa licha ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati zilizopo katika maeneo hayo pia wanauza vifaa vyake kwa lengo lakuwezesha kuwa na umeme wa kutosha.
Kampuni hiyo inayofanya kazi zake katika nchi mbalimbali zilizoendelea duniani kama Canada, nchi za bara la Asia, Ulaya na katika nchi nyingine zinazoendelea kama Brasil, Chile na Peru. Lakini sasa kupitia pendekezo la Ukanda mmoja na njia moja (BRI)iliyoasisiwa na Rais wa China Xi Jinping ikiwa na lengo mojawapola kukuza uwekezaji hasa wa viwanda Afrika ni nafasi kwa kampuni hiyo kusaidia kupatikana kwa Nishati hiyo. Nchi kama Tanzania ambayo Rais wake, John Magufuli amekuwa na Sera ya kuhakikisha inakuwa nchi ya Viwanda imekuwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na umeme wa kutosha wenye uhakika hivyo kuwa na miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme. Lakini uzalishaji huo katika nishati mbalimbali umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo DEC imesema itahakikisha inazimaliza ikiwemo kutumia Teknolojia za kisasa rafikikwa Mazingira.
kampuni hiyo imejikita katika kujenga miradi ya kuzalisha umeme katika nchi za Afrika na Tayari wanatoa huduma zao katika nchi za Angola, Zambia, Kenya na Ethiopia. Katika nchi hizo za Afrika ambazo wameanza kufanya kazi, kuna miradi iliyopo katika hatua mbalimbali kama nchini Ethiopia ambapo kampuni hiyo inajenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia upepo utakaozalisha megawati 120. Mtambo huo utajengwa katika eneo la Somali na unatarajia kuanza kujengwa mwezi Julai mwaka huu na kuchukua miezi 18 kukamilika kwa gharama ya dola za Marekani 257 ambazo asilimia 85 ya fedha hizo zitatolewa na Benki ya China Export-Import na zinazobaki zitatolewa na serikali ya Ethiopia.
Mradi huo wa kuzalisha umeme kwa upepo utakuwa wa tatu nchiniEthiopia ambapo serikali imedhamiria kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 4200 za sasa hadi 17,300 ifikapo mwaka 2020 kwa kutumia nishati mbalimbali. Nchini Kenya,Kampuni ya DEC wanatarajia kuanza ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya m awe katikaeneo la Lamu, Mombasa ambapo baada ya kukamilika itanufaisha wananchi wa eneo hilo na maeneo mengine ya Pwani ya nchi hiyo. Anasema kwa sasa wanasubiri idhini kutoka serikali ya nchi hiyo huku utaratibu wa kupata pesa ya ujenzi wa mradi huo ukiendelea vema katika Benki moja ya nchini China. Weidong anazitaka serikali za nchi za Afrika kuhakikisha wanatekeleza miradi waliyokubaliana kufanya kwa kufikia muafaka mapema kwani miradi mingi inakwama kutokana na baadhi ya serikali kuchelewa kutoa maamuzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |