Na Theopista Nsanzugwanko,Inner Mongolia-China
Ordos ni mji maarufu katika eneo la Mongolia nchini China huku kukiwa na maeneo mengi ya kihistoria yanayoelezea historia,viongozi na imani ya watu wa eneo hilo ikiwa ni njia ya kudumiasha mila na tamaduni zao.
Hekalu moja lililopo katika mji huo limekuwa kivutio kwa maelfu ya watalii na wafuasi wa kiongozi kutoka Mongolia ambaye alitawala zaidi ya miaka 800 yaliyopita.
Kiongozi huyo wa Mongolia,Chingis Khan amekuwa katika hekalu hilo linaloonesha umaarufu wake kutokana na tabia zake wakati wa vita mbalimbali.
Historia inaonesha kuwa ,Khan maarufu katika eneo hilo kama 'Temujin' inakadiliwa aliuwa zaidi ya watu milioni 40 kati ya mwaka 1206 hadi 1227 katika mapigano na zaidi ya mataifa 40 katika eneo la mita za mraba milioni 12.
Lakini kwa watu wa jamii hiyo ya Mongolia na makundi mengine ya kijadi kaskazini mwa nchi ya China ,wanajivunia Genghis Khan, aliyekufa miaka 800 iliyopita na kuendelea uwa mtu wa kuheshimika na mfano wa kuigwa .
Pembeni mwa sehemu ulipohifadhiwa mwili wake katika mji huo wa Ordos kumejengwa minara ya Genghis Khan ya kila aina mbalimbali ambapo wafuasi wake wanaenda kuabudu na kutoa sadaka.
Aidha sanamu zake zimekuwa maarufu sana kwa nyumba binafsi na maeneo ya umma.
Sehemu moja inayokuwa kwa sana katika jiji lile imepewa jina kutokana na maisha yake huku wengine wakifichua kuwa Khan anaabudiwa na kuchukuliwa kama Mungu.
Nikiwa mmoja wa waandishi wa habri 27 kutoka nchi za Afrika,waliotembelea eneo hilo lililohifadhiwa mwili wake tulishuhudia minara ya mishumaa inayowaka na mbele yake kukiwa na idadi kubwa ya walinzi ambao ukesha kulinda eneo hilo,nyakati zote.
Wafuasi wake wamekuwa wakiamini kuwa watabarikiwa kwa kutembelea maeneo hayo.
Mbali na wafuasi kutembelea na kuabudu pia hutoa maombi yao kwa masuala mbalimbali yanayowakabili wakiamini kupatiwa ufumbuzi.
Lakini pia katika hifadhi hiyo pia kuna vifaa mbalimbali vilivyotumika wakati huo kama vyombo,silaha ,nguo na nakala za ripoti mbalimbali .
Mlinzi wa kike katika eneo hilo,Wagier Qaqi,anaeleza kuwa Genghis Khan alikuwa ni mtu mwenye siri sana kiasi ambacho hakukubali kupigwa picha .
Anasema picha pekee iliyopo katika makumbusho hiyo ni iliyochorwa kwa kuzingatia muonekano wake ulivyokuwa kutokana na maelekezo yaliyotolewa na wasaidizi wake mara baada ya kufariki dunia.
Qaqi anaeleza kuwa hifadhi hiyo ya mwili wa Khan inapokea wageni 200 hadi 8,000 kwa siku katika vipindi tofauti.
Naye,mmoja wa walinzi 30 wanaolinda eneo hilo usiku na mchana, Ji Ran Ba Ya Er, (54) anasema moja ya kazi zao ni kuhakikisha kuwa hakuna mgeni anayepiga picha ndani ya hekalu hilo.
Pia mlinzi huyo aliyefanya kazi ya ulinzi katika hekalu hilo kwa miaka zaidi ya 10 anasema pia wamekuwa na kazi ya kuwasha mishumaa katika eneo hilo na kulinda funguo na vitabu vya Genghis Khans,vilivyohifadhiwa .
Anasema yeye na wenzake wamekuwa wakilipwa yuan 4,000 kwa mwezi kutokana na kazi hiyo ya ulinzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |