• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waandishi wa habari  China   wataka Afrika iangaziwe zaidi

    (GMT+08:00) 2017-08-09 14:29:23

    Na Theopista Nsanzugwanko,Beijing ,China

    WIKI iliyopita waandishi wa habari kutoka China na Afrika walikutana kwa mualiko wa taasisi ya kimataifa ya Sino-Africa Watch,(ISAW) walioandaa mkutano maalum kwa waandishi wa habari hapa Beijing kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya China na Afrika.

    Mkutano huo ni wa tatu tangu kuundwa kwa ISAW ambayo ni taasisi ya waandishi wa habari wa China mwaka 2014 na kuhudhuliwa na watu zaidi ya 30 wakiwemo waandishi wa habari wa China wengine kutoka Afrika.

    Pia wasomi, wawekezaji, mameneja katika kampuni mbalimbali pamoja na washauri katika masuala mbalimbali kuhusu China na Afrika kutoka pande hizo mbili walihudhuria,

    Wataalamu mbalimbali wa masuala ya ushirikiano Afrika walizungumza akiwemo Lingxiu Zhang ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Afrika aliyesema wawekezaji wa China wana fursa za kuwekeza Afrika katika kilimo, miundombinu, viwanda, afya na maendeleo ya utandawazi.

    Aliyewahi kuwa Mwandishi wa habari katika kituo cha luninga cha China Central Television, CCTV sasa China Global Television Network, CGTN Fei Yu alizungumza katika mkutano huo na kujiuliza ni nini kitafuata kwa wawekezaji wa china walio Africa baada ya kumaliza ujenzi wa mabwawa,barabara, madaraja na ujenzi wa miundombinu na miradi mingine muhimu.

    Ataka ufike wakati wafanyabiashara kutoka China walioko Afrika kufanya biashara kama wafanyabiashara raia wa India ambao wanafanya biashara endelevu kwa familia,inayorithiwa kizazi mpaka kizazi.

    Mtafiti na mwandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha London,ambaye pia ni mwanachama wa ISAW,Hangwei Li anasema mkutano huu ni muhimu katika kujenga mahusiano.

    Alisema ni muhimu kwa sababu unawaweka pamoja wasomi wa kutoka China pamoja na Waandishi wa habari kutoka Afrika na China, watendaji kutoka serikalini na mameneja wa kampuni mbalimbali.

    Anasema ushirikiano ni muhimu kwa China na Afrika kwa kila upande kufahamiana vizuri kwani China ni mshirika mkubwa wa biashara na Afrika na kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni kwa mujibu wa kampuni ya Mckinsey kuna mamilioni ya wachina wanaishi Afrika.

    Mkutano huo unawezesha wadau mbalimbali kuelewa vizuri kuhusu China na Afrika.

    "matatizo mengi ya wachina wanapokuwa Afrika wakati mwingine ni kutokana na mawasiliano mabovu,kwa wachina kutowaelewa vizuri waafrika pia na waafrika kutowaelewa vizuri wachina'Alisema

    Anasema lakini kwa nyakati zijazo ,anaamini kuwa China na Afrika watakuwa na ushirikiano mzuri zaidi, hususan chini ya pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ambapo kuna fursa nyingi za uwekezaji kwa makampuni ya China kuwekeza Afrika, kama vile kulivyo na nafasi nyingi kwa wafanyabiashara wa Afrika kufanya biashara nchini China.

    Naye Jingwei Zhang kutoka Taasisi ya mazingira duniani anasema ana furaha ya kuwasikiliza watu wanaofanya kazi nje ya nchi kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji barani Afrika, na kuwa amevutiwa na Lingxiu Zhang aliyezungumzia kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika.

    Naye, mwandishi wa habari za siasa na mambo ya nje kutoka CGTN, Su Yuxing, anasema amekuwa akiandika habari mbalimbali kuhusu mahusiano ya China na Afrika na katika majadiliano ya mkutano huo amebaini pande zote mbili zina hamasa katika kudumisha mahusiano.

    Anaeleza kuwa uzoefu alioupata kwa waandishi wa habari wa China kufanya kazi Afrika hasa kuhusu mkutano wa Ushirikiano kati ya China-Afrika(FOCAC) uliofanyika Afrika Kusini Mwaka 2015 na Rais wa China Xi Jinping kuzungumzia ushirikiano wa pande hizo mbili.

    "katika mkutano huo nilimhoji rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye alisema baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi wana mtazamo tofauti kuhusu mahusiano ya China na Afrika, hivyo kunatakiwa pande hizo mbili kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu uhusiano wao"anasema

    Mugabe aliendelea kusema kama utasikiliza vyombo vya magaharibi kuhusu taarifa zao za China, hawakupi picha halisia ya nchi hiyo hivyo ni vigumu kuelewa China labda ukipata nafasi ya kutembelea na kupata uzoefu wa kila jambo linaloendelea.

    Su anashauri kuwa China imekuwa na mageuzi mbalimbali na kutaka Afrika na China hawakutani kujadiliana masuala ya siasa na uchumi lakini pia kuimarisha uhusiano na kubadilishana uzoefu baina ya watu wake.

    Waandalizi wa mkutano huo wanaeleza lengo lao ni kuondoa uelewa hasi wa wachina kuhusu Afrika kwa kuanzisha mijadala ya wazi ya wataalamu kuhusu masuala ya China na Afrika.

    ISAW, imeundwa mwaka 2014 na wanahabari kutoka China na imekuwa uwanja mpana unaofuatiliwa mtandaoni na waandishi wa habari na watafiti 25 na mpaka sasa imezalisha zaidi ya nakala 100 za waandishi,mapitio ya vitabu na kutoa matangazo zaidi ya 10 yanayohusu uchaguzi wa marais wa Afrika, habari kuhusu Wachina walioko Afrika na waafrika walioko China pamoja na habari mbalimbali za wiki kwa ufupi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako