• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi kuupa kipaumbele mfumo wa Ukanda mmoja Njia moja katika awamu yake ya pili madarakani

    (GMT+08:00) 2017-10-21 15:48:48

    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    WIKI hii macho na masikio duniani yalielekezwa nchini China kunakofanyika Mkutano Mkuu wa 19 wa chama cha kikomunisti cha CPC,kinachotawala nchini hapa.

    Katika mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe 2,307 huku ukifuatiliwa kwa karibu za vyombo vya habari zaidi ya 3000,umekuwa gunzo kubwa hususan baada ya msemaji wa Chama hicho kuweka wazi Agenda za Mkutano huo.

    Mbali na kujadiliana masuala mbalimbali ya Maendeleo ya kichumi,kisiasa na kijamii,msemaji wa mkutano huo mkubwa kichama Tuo Zhen,anaeleza kuwa mbali ya kujadili mabadiliko ya katiba ya Chama hicho pia watachagua wajumbe wa kamati mbalimbali za chama hicho.

    Katika Mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka mitano, ni hitimisho la utawala wa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping kwa awamu ya kwanza na kwa mujibu wa katiba kumuweka wazi mrithi wake wa nafasi ya urais baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10.

    lakini mkutano huo umekuwa na mvuto zaidi pale alipoweka wazi kazi alizofanya kwa miaka mitano iliyopita na vipaumbele kwa miaka mitano ijayo.

    Akifungua mkutano huo,mbali na kuelezea mafanikio yake katika ushirikiano wa aina mbalimbali duniani,,uboreshaji wa huduma za wananchi wake kwa kuwaondoa katika umasikini huku akipambana na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vimeshamiri,ukuaji wa uchumi na mengineyo pia ameelezea ushirikiano wake na nchi zinazoendelea duniani zikiwemo zile za Afrika.

    Kupitia,mfumo wake aliouasisi mwaka 2013 na kuzinduliwa mwezi Mei mwaka huu,Rais Jinping katika awamu ya pili ya utawala wake amehaidi kuwekeza zaidi fedha na Rasilimali kwenye mfumo unaoongozwa na serikali yake wa mkanda mmoja , njia moja (One Belt and One Road Initiative , OBOR).

    Taifa hilo lenye uchumi mkubwa wa pili Duniani,katika mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo waliwekeza zaidi ya Dola za Marekani bilioni 100 kwa lengo la kukuza ushirikiano hususan katika kupanua na kuinua viwango vya miundombinu ,biashara,ufadhili wa miradi na kubadilishana Teknolojia hasa katika mataifa yanayoendelea Afrika ikiwemo Tanzania.

    Xi ameeleza kuwa katika utawala wake wa awamu ya pili,China itaweka mipango madhubuti kuhakikisha kwamba taifa hilo litaunganisha mataifa mengi duniani kupitia mfumo huo ambao kwa sasa una zaidi ya wanachama 68 kutoka mataifa na taasisi za kimataifa.

    "tutaupa kipaumbele mfumo wa mkanda mmoja na njia moja na kusisitiza ukuaji wa pamoja kwa kutumia majadiliano na ushirikiano,kwa kuongeza uwazi ,ushirikiano kwa kuinua viwango vya ubunifu"alisema

    Anasema kuwa watapanua biashara na nchi za kigeni ,kuanzia aina na mifumo mipya ya kibiashara huku wakihakikisha China ninakuwa nchi ya biashara zenye viwango.

    "tutatengeneza sera kuhamasisha viwango bora vya uwekezaji na kuhakikisha wafanyabiashara wote waliosajiliwa nchini China wanahudumiwa kwa usawa"anasema na kusisitiza kuwa huru kwa kanda zote katika kufanya biashara.

    Wakati huo huo, wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti (CPC) wamesifia wito huo wakieleza kuwa ni bora zaidi katika mahusiano ya China na Mataifa rafiki.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo ambaye pia ni mjumbe wa CPC,Wang Yi anasema mfumo huo unawakilisha mawazo na mitazamo ya Wachina kwa ujumla na kuwa mradi mmoja uliopewa kipaumbele katika serikali ya awamu ya kwanza ya Rais huyo kwa miaka mitano iliyopita.

    "mfumo huu wa OBOR ni mojawapo ya wazo mahususi kutoka kwa taifa letu,kwa kuwa inadhihirisha fikra na ndoto za maelewano na mafanikio kwa kila upande"anasema Wang

    Waziri huyo anaeleza kuwa mfumo huo unaonyesha kwa jinsi China inavyohusika kwa kiasi kikubwa na mambo ya ulimwengu kwa kutaka kuboresha maisha ya kila sehemu.

    Katika uzinduzi wa mfumo huo uliohudhuriwa na wakuu wan chi na maafisa serikalini 28 ulihudhuriwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta,Waziri Mkuu wa Ethiopia,huku Tanzania ikiwakilisha na waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa.

    Mfumo huo wa Rais Xi kwa mwaka 2013, lengo lake kuimarisha mtandao wa biashara na Miundombinu na kuunganisha nchi za the Asia ,Ulaya na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako