• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya kutengeneza magari ya umeme kutoka China inapanga kuwekeza zaidi Afrika

    (GMT+08:00) 2017-11-18 16:51:25

    Na Eric Biegon mjini Beijing, China.

    Serikali ya China inasema kuwa ina nia ya kuondoa magari yote yanayotumia mafuta kwenye barabara zake katika miaka michache ijayo. Badala yake magari yanayotumia nishati ya umeme yatachukua nafasi yao, ambayo Beijing inasema inatokana na mahitaji makubwa nyumbani na nje ya nchi.

    Hadi sasa, ndani ya kipindi kifupi, China imejulikana kama kiongozi katika utengenezaji na uuzaji wa magari yanayotumia umeme. Kampuni ya Kichina, Beijing Automotive Industry Corporation-Beijing Electric Vehicle Company, maarufu BAIC-BJEV, inasema iliuza magari mapya ya nishati takriban nusu milioni mwaka jana peke yake.

    Hii ndio sababu China inaamini kwamba ipo njiani kutekeleza lengo lake la kuwa na jamii yenye kutumia magari ya umeme kikamilifu.

    Makamu wa Rais Mtendaji wa BAIC Li Xingxing, anasema utumizi wa magari ya umeme ni wazo nzuri kwa wakati huu kwani hayana hathari za kuchafua mazingira.

    "Faida ya magari mapya ya nishati ya umeme ni pamoja na wajibu wa kijamii ambao ni kutunza mazingira kwa kutochafua. Magari hayo pia ni ya gharama nafuu ya matengenezo, na teknolojia ambayo ni msingi wake." Bwana Li akasema

    Katika taarifa iliyochapishwa na kampuni ya uchapishaji ya Electrek, China ilizalisha kwa mara mbili magari yanayotumia umeme kufikia 600,000 mwaka uliopita, zaidi ya Marekani na mataifa ya Ulaya kwa pamoja.

    "Soko la NEV la China lina zaidi ya miundo 60, ambapo 13 kati yao yaliuza zaidi ya magari 10,000 katika 2016." Uchapishaji huo ulibainisha.

    Makampuni ya Kichina yanasema yaliafikia viwango hivyo kutokana na uwekezaji mkubwa hasa katika utafiti na maendeleo.

    "Sisi tunatumia sayansi na teknolojia kama msingi wa shughili zetu ikilinganishwa na wengine. Makao makuu yetu ya Blue Park mjini Beijing ni kitovu cha ubunifu. Tuna mpango wa kujenga vituo 7 vya R&D kote duniani." Akasema Katibu wa BAIC Lian Qing Fang.

    Kuwekeza katika Afrika

    Usimamizi wa BAIC BJEV inasema ina mpango wa kupanua biashara yake kwa nchi zaidi. Tayari kampuni hiyo imeanzisha kiwanda nchini Afrika Kusini na inafanya biashara katika nchi 48, ikiwa ni pamoja na Sudan, Ghana, Misri, Angola na Ethiopia.

    Kampuni hiyo inasema imewekeza milioni 826 dola za Marekani katika uanzishwaji wa kiwanda chake Afrika Kusini. Magari ya kwanza kutoka kiwanda hicho yanatarajiwa mapema mwaka ujao, na asilimia kubwa ya magari hayo yatauzwa barani Afrika.

    Kiwanda hicho kilichoko karibu na kitovu cha kuuza magari ya Port Elizabeth, itakuwa kiwanda cha magari cha kwanza katika Afrika Kusini ndani ya miongo minne. Kiwanda hicho kinatarajiwa kutengeneza magari 50,000 kufikia mwaka 2022, ambayo ni nusu ya idadi inayolenga ya 100,000.

    BAIC iliingia ubia pamoja na shirika la maendeleo la viwanda ya Afrika Kusini na na kapuni hiyo imetoa hakikisho la upatikanaji wa vipuri au spea katika Afrika.

    BAIC inatazamia kuzidisha uwezo wake wa kuzalisha magari yanayotumia umeme wa 800,000 kila mwaka. Kampuni hiyo ina mfululizo wa bidhaa aina tano, pamoja na baadhi ya magari ya kwenda kilimota 400 baada ya kuchaji mara moja.

    Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China inaonyesha kwamba sekta mpya ya magari ya nishati ya umeme China imeshuhudia upanuzi imara kuanzia mwaka 2009, na kuwa soko kubwa ya magari hayo duniani tangu mwaka 2015.

    Kampuni ya ushauri kutoka Ujerumani iliunga mkono matokeo ya utafiti huu na kutabiri kwamba China itakuwa na jukumu kubwa katika maendeleo ya baadaye ya sekta ya kimataifa ya NEV, kutokana na ukuaji wake imara wa soko.

    Ama kwa kweli, shirikisho la magari ya abiria China, CPCA, kinasema makampuni ya kielectroniki ya kutoka China zikiwemo BYD, BAIC na Geely, ziliorodheshwa pamoja na makampuni makubwa duniani katika suala la mauzo ya magari yanayotumia umeme katika mwaka 2016.

    Chama cha watengenezaji magari China kinakadiria kwamba mauzo ya magari hayo ya NEV yatafikia vipande 800,000 mwishoni mwa mwaka huu. Chama hicho kinasema mafanikio hayo yanatokana na msaada wa serikali na taratibu rahisi za kupata leseni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako