• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfanyabiashara maarufu kutoka China kuanzisha viwanda ndogo ndogo Afrika

    (GMT+08:00) 2017-11-22 19:31:00
    Mfanyabiashara maarufu kutoka China kuanzisha viwanda ndogo ndogo Afrika

    Na Eric Biegon katika Beijing, China.

    Mfanyabiashara kutoka China ametangaza mpango wa kupanua biashara zake barani Afrika kwa kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo tano kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za nyumbani za matumizi ya kila siku kama vile betri za tochi, karatasi ya choo na bidhaa za elektroniki.

    Yiqiao Yin, anayefahamika sana kama George Yin, amefichua kuwa ana mpango ya kuzindua kiwanda cha kwanza mwaka ujao nchini Msumbiji. Aidha kulingana naye viwanda vingine nne vidogo vilivyobaki vitaanzishwa katika mataifa ya Afrika nne kati ya saba ambapo makampuni yake tayari yanazalisha madirisha na milango kutoka alumini.

    "Kila kiwanda ndogo kitaajiri watu angalau 1,000 kwa gharama ya takriban milioni 50 dola za Marekani," Yin alielezea.

    Kampuni yake kufikia sasa imewekeza milioni 100 dola za Marekani katika nchi saba za Afrika katika miaka 20 iliyopita. Yiqiao Yin anasema yuko tayari kuwekeza katika nchi zaidi za Afrika iwapo serikali zitatoa motisha ya kutosha.

    Akiudumu zamani kama mhadhiri wa somo la hesabu katika chuo kikuu, Yin alijiuzulu nafasi yake na kuanza biashara yake mwenyewe. Leo, yeye ni Meneja Mkuu wa Future Group, FGC, na Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara kutoka mkoa wa Hubei katika Afrika, HCCA. Amekuwa akifanya biashara katika Afrika kwa miaka 20 baada ya kubuni biashara yake ya kwanza nchini Madagascar mwaka 1998.

    Yin anazalisha alumini ya madirisha, milango, vibanda na mapambo mengine ya ujenzi, na kuajiri wafanyakazi zaidi kutoka mataifa anamofanya biashara yake. Yeye pia anashiriki katika miradi ya ujenzi na mapambo, biashara ya bidhaa za ujenzi na biashara ya mali isiyohamishika.

    Kiwanda chake kilichoko Madagascar kwa sasa ni kubwa na maarufu zaidi katika uzalishaji wa alumini nchini humo, akitawala takriban asilimia 40 ya soko ya bidhaa hiyo. Amefanikiwa kujenga matawi katika kila mkoa na maduka 10 katika mji mkuu, Antananarivo.

    Kwa jumla, biashara ya Yin ya kuuza alumini imenawiri katika nchi saba za Afrika zikiwemo Madagascar, Kenya, Tanzania, Uganda, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Angola. Makao makuu ya biashara yake ya Afrika ni Nairobi, Kenya.

    Mfanyabiashara huyo amefichua kuwa FGC inaajiri watu wapatao 2,000 katika nchi hizo saba, pamoja na takriban wafanyakazi 200 wa Kichina. Hata ingawa Yin hakutaka kuzungumzia pato la kampuni yake kutokana na mauzo ya kila mwaka, yeye anasema FGC ingali inakuwa.

    "Ikilinganishwa na viwango vya China, soko la Afrika bado ni ndogo, hivyo kampuni yangu pia ni ndogo. Nataka kuanzisha kanda ndogo ya viwanda Afrika kwa sababu China ni kituo cha viwanda duniani na kwa sasa wafanyabiashara wengi kutoka China wameanza kuwekeza nje ya nchi. Afrika ni nzuri kwa uwekezaji kwani soko lake bado ni linaongezeka." Yin alielezea.

    Makao makuu ya kampuni yake ya Future Group nchini China yamo Wuhan, katika mkoa wa Hubei. Anamiliki makampuni mengine matatu tanzu nchini, ikiwa ni pamoja na ya usafirishaji wa nje na kituo cha ugavi katika mikoa ya Wuhan na Foshan mtawalia.

    Yin anasema Future Group inakuza thamani za "kushiriki na kukua kwa pamoja" na kutekeleza majukumu ya kijamii kwa kufuata kanuni ya kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi ambapo makampuni yake yanafanya biashara.

    Anasema amesaidia kukuza zaidi ya vipaji 200 kutoka Afrika kwa ajili ya usimamizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako