• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waafrika wanaohitimu mafunzo China kupatiwa ajira.

    (GMT+08:00) 2017-11-22 19:39:57

    Waafrika wanaohitimu mafunzo China kupatiwa ajira.

    Na Theopista Nsanzugwanko mjini Beijing

    TATIZO la ukosefu wa ajira kwa vijana katika nchi za Afrika hasa wanaohitimu masomo katika vyuo vikuu mbalimbali limekuwa kubwa hivyo kuathiri uchumi wa nchi hizo zinazoendelea duniani kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mifumo ya elimu inayowaandaa wengi kuajiliwa na siyo kujiajiri.

    Inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya wanafunzi wanaohitimu katika vyuo vikuu zaidi ya 668 Afrika wanakosa ajira.

    Serikali za nchi hizo zimekuwa zikiweka mikakati mbalimbali ya kuweza kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kujenga mazingira ya kuweza kujiajili lakini bado haijaweza kuzaa matunda kwa kiasi kikubwa.

    Katika kukabiliana na changamoto hiyo,kupitia ushirikiano wa nchi za Afrika na China,wanafunzi wanaosomea taaluma mbalimbali nchini humo wamepatiwa fursa ya kupata ajira kutoka makampuni mbalimbali .

    inakadiliwa kuwa kuna wanafunzi 60,000 wanaendelea na masomo mbalimbali kutoka mataifa ya nje nchini wakiwemo wanaotoka nchi hizo za Afrika huku wengi wao wakipatiwa ufadhili na serikali ya China.

    Wiki iliyopita kulifanyika maonesho yaliyoandaliwa na

    Shirikisho la ushirikiano wa China na mataifa ya nje (CPAFFC),kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumi (UIBE) cha Beijing kwa lengo la kuwapatia Ajira wahitimu kutoka Afrika wenye taaluma mbalimbali.

    Waandaaji hao wameandaa kanzidata kwa ajili ya kutengeneza ajira kwa wanafunzi wa Afrika wanaohitimu nchini humo kupata katika maonesho yaliyofanyika Novemba 15 mwaka huu.

    Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika na Asia katika taasisi ya CPAFFC ,Xu Yan anaelezea kuwa maonesho hayo yamewapa mwanga mpya kutokana na kuwa ni mara yao ya kwanza kuandaa.

    Anaeleza kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ya siku moja ilikuwa ni 'mfumo wa Ukanda mmoja Njia moja na matarajio ya upatikanaji wa Ajira kwa vijana wa Afrika'

    Anasema maonesho hayo yamehudhuliwa na kampuni zaidi ya 60 za kichina zinazofanya kazi nchini China na Afrika na kutembelewa na wanafunzi zaidi ya 400 wa kiafrika.

    Pia wanadiplomasia na viongozi wa taasisi za ushirikiano wa nchi mbalimbali za Afrika na China kutoka nchi mbalimbali nao walipata fursa ya kutembelea maonesho hayo ambayo CPAFFC na UIBE walisaini makubaliano ya ushirikiano katika maonesho mengine kama hayo kwa miaka ijayo.

    Makamu wa Rais wa taasisi ya Ushirikiano baina ya Zimbabwe na China ,Mandi Chimene,anasema maonyesho hayo ambayo kiwango cha chini cha kupata ajira ni elimu ya shahada ya kwanza inatoa matumaini kwa wanafunzi kuajiliwa nchini humo baada ya kuhitimu.

    Chimene ambaye pia ni Gavana wa jimbo la Manicaland nchini Zimbambwe amewataka vijana wa Kiafrika kusoma kwa bidii na kuwa mabalozi wazuri pale watakapopata kazi ili kutoa nafasi ya wengi zaidi kupata nafasi hiyo.

    "lakini pia kuwa mbali na nyumbani siyo nafasi ya kufanya kile mnachotaka au kilicho tofauti na mila na Desturi za nchi zenu ni vema kulinda tamaduni zenu za kiafrika na kusoma kwa bidii kuhakikisha mnamaliza masomo kwa amani"anasisitiza

    Naye,Waziri wa Zamani wa Sudani Kusini ,Dk Barnaba Benjamin, ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Ushirikiano baina ya China na Sudan Kusini anasema maonesho hayo yanasaidia vijana wa Afrika kuwa na matarajio makubwa mapema baada ya kumaliza mafunzo hayo.

    "elimu bora na mafunzo mliyopata kutoka China inawaandaa kwa ajili ya majukumu makubwa katika bara letu ambalo bado liko nyuma kimaendeleo ,kwa kuwa maonesho haya yanawaandaa na kuwapa mtazamo mpya wa kufanya mara baada ya kurejea nyumbani "anasema Benjamini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako