Majaliwa Christopher
WAZIRI Mkuu wa China Bw. Li Kequiang mapema leo ametoa ripoti juu ya utendaji wa serikali katika miaka mitano iliyopita.
Ni miaka ya mafanikio makubwa, katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Lakini, zaidi ya yote, ni ripoti iliyodhihirisha namna ambavyo China inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo huku ikiimarisha mahusiano yake na nchi zingine.
Kwa mujibu ya ripoti hiyo, China imeweka rekodi ya kipekee sana, pato la taifa likikuwa kutoka yuan trilioni 54 hadi trilioni 82.7 huku mchango wa nchi katika maendeleo ya dunia ikizidi asilimia 30.
Hili la kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa dunia inaipa China nafasi ya kuwa moja kati ya nchi zenye marafiki wengi sana huku ikiimarisha uhusiano wake wa diplomasia ya kiuchumi.
Bw. Li ametaja maeneo yaliyopata maendeleo chanya kuwa ni kuimarika kwa maisha ya wananchi, kupungua kwa uchafuzi wa mazingira, kukua kwa biashara baina ya China na nchi zingine na makusanyo yakiongezeka kutoka yuan trilioni 11.7 hadi kufikia 17.3 trilioni.
Mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi hiki kwa mujibu wa waziri mkuu ni umaskini kwa mtu mmoja mmoja kupungua kutoka asilimia 10 .2 hadi kufikia asilimia 3.1 huku watu milioni 68 wakiokolewa kutoka kwenye dimbwi la umaskini.
Kwa kipindi hiki pia China, ilishuhudia kukua kwa shughuli za biashara, kuongozeka na kuboreka kwa miundombinu na mafanikio makubwa sana katika mradi wa Ukanda Mmmoja, Njia Moja pamoja na kuimarika kwa utalii.
Baada ya kuelezea mafanikio yalipatikana ndani ya muda huu, Bw. Li pia amezungumzia na kugusia maeneo muhimu ambayo kama nchi watayapa kipaumbele kuhakikisha China inaendelea kuwa nchi bora, salama na unaostawi kwa manufaa ya wanachi wake na nchi marafiki duniani.
Baadhi ya maeneo yatakayopewa msukumo wa kipekee ni ubunifu na utafiti ambayo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuangalia upya gharama za mitandao ya simu, kuendelea na programu za kuboresha maisha ya wananchi, kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji pamoja na kupitia upya mifumo ya kodi.
Taarifa aliyoitoa waziri mkuu, inaashiria kuwa China inatekeleza mipango yake kwa vitendo na hii inatokana na kuwa na serikali thabiti ambayo huweza kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali inayopitishwa na Bunge la Umma.
Pamoja na maendeleo makubwa ambayo China imeweza kuyapata, lakini bado imebaki kuwa moja kati ya nchi zenye mchango mkubwa sana katika maendeleo na ustawi na nchi zinazoendelea.
Ni taifa kutoka bara la Asia Mashariki linaongoza kwa kufadhili miradi mbalimbali kama vile afya na elimu katika nchi nyingi za dunia ya tatu.
Takwimu zinazoeonyesha kuwa mchango wa China katika maendeleo ya dunia huzidi asilimia 30, imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano uliopo baina yake na nchi zingine.
Mahusiano hayo ya kutolewa mfano, umechangia pia kukuwa kwa shughuli za biashara na miradi mbalimbali yenye faida kwa pande zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |