Na Theopista Nsanzugwanko, Dar es Salaam, Tanzania
WIKI hii China imeingia katika historia mpya baada ya Rais wa nchi hiyo Xi Jinping kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo katika muhula mwingine.
Hatua hiyo imefuatiwa baada ya Bunge la Umma kupitisha mabadiliko ya Katiba na kuondoa ukomo wa muda wa urais ambao awali ulikuwa mihula miwili.
Katika kuonesha maamuzi hayo yamekuwa wakati muafaka na yenye busara kutokana na yale aliyozungumza wakati wa kufunga Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China,huku akiwa tayari kuingia muhula mpya.
Ikiwa ni hotuba yake ya kwanza tangu kufanyika kwa maamuzi hayo makubwa ya nchi ameonesha fahari katika kuongoza kwa kutumia wananchi zaidi huku akihakikisha nchi hiyo inazidi kusonga mbele kimaendeleo.
Akiwa na sera ya kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi zingine duniani huku serikali ikisisitiza usawa na faida kwa wote katika njia zake za ushirikiano na mataifa makubwa na yale machanga mengi yake yakitokea Afrika.
Kutoka na dhana yake ya kufika mbali kimaendeleo na kusimamia maslahi ya nchi hiyo katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii, Bunge la Umma la China lilimpitisha kwa umoja wao.
Kwa muda wote wa utawala wake, yaani miaka mitano kumekuwa na mabadiliko ya masuala mbalimbali ya miundombinu, diplomasia pamoja na ushirikiano na nchi mbalimbali duniani.
Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kufanyika maamuzi hayo, anaweka wazi malengo yake katika ustaarabu wa China, upendo kwa wananchi, imani thabiti kwa maendeleo ya China na matumaini ya kuwanufaisha binadamu.
Msingi wake mkubwa katika utawala wake, Rais huyo anabainisha kuwa ni kuhudumia watu huku akiwahakikishia kuwa majukumu aliyopewa na katiba atayafanya kwa uaminifu.
Alibainisha kuwa ataendelea kuwatumikia watu akikubali kusimamiwa na watu huku akihaidi kutowasaliti wananchi wa China kutoka makabila mbalimbali.
Xi anawataka watendaji wa vyombo vya serikali kufanya kazi kwa kuweka maslahi ya wananchi kwanza kwa kuwahudumia na kufanya kazi kwa bidhii kutokana na mahitaji na furaha za wananchi.
Katika hotuba yake, Xi anasema wananchi wa China ni wabunifu wakubwa na kuamini kuwa watu zaidi ya bilioni 1.3 wakiendeleza ubunifu wao nchi hiyo iteonyesha miujiza kila wakati.
Pia alisema wananchi wake ni wapambanaji katika kila sekta hivyo anaamini nchi hiyo itafikia malengo yake ya kuwafanya wawe na maisha bora. Alisema pia kwa umoja walionao watu hao pamoja na ari ya kufikia malengo waliojiwekea itasaidia kufikia mbele zaidi malengo yao.
Alisema nchi hiyo iko kwa ajili ya watu wake, hivyo lazima kuelekeza nguvu zake katika mahitaji ya watu, kuhakikisha kujifunza kwa unyenyekevu kwa watu, kutumia mahitaji yao na kujifunza busara kutoka kwao.
Akaeleza ana imani maendeleo zaidi China, na kuwataka kila mmoja kuendana na historia mpya ya China kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Alieleza kuwa uongozi wa Chama cha kikomunisti cha China inaendana na ujamaa na Tabia za kichina.
Hakika kutokana na tukio hilo na msisitizo wa Rais Xi katika utawala wake unaoendana kwa matakwa ya wananchi wake ni jambo linaloweza kujifunza kwa mataifa mengine kwa lengo la kuondoa migogoro ya wananchi kuhusu kujipatia huduma muhimu.
Katika kuendana na Demokrasia kwa watu wake, Taifa hilo kubwa duniani limewezesha kuwa na demokrasia ya pekee katika mfumo wa ujamaa unaendana na nchi hiyo kuongozwa na chama kimoja lakini kimejenga umoja na mshikamano baina yao.
Kutokana na umoja na mapendekezo yake ikiwemo mikakati mbalimbali iliyowekwa na Rais huyo tangu kuingia madarakani inaonesha kuimarisha zaidi ushirikiano wa kidplomasia na mataifa mengine duniani ikiwemo nchi za Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |