• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kushirikisha vyombo vya habari vya nchi mbalimbali kwa kuhimiza mazungumzo ya ustaarabu

    (GMT+08:00) 2018-04-10 14:02:45
    na Trix Ingado Luvindi, Sanya, China


    Jamii ya vyombo vya habari barani asia hii leo imehimizwa kutilia mkazo usambazaji wa taarifa zitakazo kuza uhusiano bora kati ya nchi za bara Asia.

    Hii ni kulingana na Bwana Huang Kunming aliye mkuu wa kamati ya Central Commitee Publicity Department nchini China alipohutubia wakuu wamashirika ya habari barani asia katika kongamano lililong'oa nanga hii leo mjini Sanya.

    Bwana Huang alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kutoa taarifa zinazo heshimu asili na tamaduni za wanaasia huku zikiangazia tamaduni tofauti za mbalimbali.

    Alisema kuwa kupitia azimio la kujifunza na kufunza, vyombo vya habari vitaweza kuleta uelewano kati ya Uchina na bara asia na dunia nzima, jambo ambalo linaambata na azimio la Rais Xi Jinping la ushirikiano wa kiuchumi kati ya Uchina na nchi za nje.

    Matamshi yake yalingwa mkono na wanahabari tofauti, akiwemo mkurugenzi mkuu wa Pakistan Broadcast Corporation ambaye alisifia mradi wa ukanda mmoja njia mmoja huku asisema, utangazaji bora utakuza ushirikiano kati ya nchi mbalimbali barani na kukuza bishara itakayo imarisha uchumi wa eneo hili la dunia.

    Mbali na hayo Bw. Jalil pia alidokeza kuwa ushirikiano wa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya vyombo vya habari itasaidia katika azimio la mradi wa ukanda mmoja njia moja kwa kusambaza taarifiza nzuri zinazo elimisha umati kuhusu utelekeleza na umuhimu wake.

    Haya ni maneno yaliyoungwa mkono na waliohudhuria kongamano wengi wakisena ushirikiano wa aina hii haufai tu barani Asia bali duniani nzima, jambo linalowezekana kupita utumizi wa mtandao na mitandao ya kijamii.

    Ili kusaidia katika azimio la maendeleo barani, ni muhimu kwa vyombo vya habari kuongoza mazungumzo na majadiliano yatakayo saidia raia kuelewa azimio la maendeleo barani na vile utangamano utasaidia katika kuleta maendeleo.

    Xinhua News Agency ilisifiwa kataka kongamano hilo la wanahabari kwa juhudi zake za kusaidia katika utangamono na kutoa habari zitakazo saidia kueneza taarifa sahihi kuhusu Asia.

    Mhariri mkuu wa China Daily alisisitiza kwamba gazeti China Daily itatilia mkazo juhudi za kuendeleza azimio la Rais Xi Jinping kuwa na jamii ya ujamaa iliyo na vipengele vya kichina.

    Alisema kuwa ni jukumu la wanahabari kusambaza taarifaa za kiundani zitakazo hakikisha kuwa dunia inaelwa tamaduni za bara hiki, kando na hayo, alihimiza kuwa wanahabari wa bara asia wanastahili kukumbatia utumizi wa mitandao katika shughuli ya kueneza taarifa nzuri kuhusu eneo hili la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako