jicho180414
|
App moja ya kuita teksi nchini China iitwayo "Usafiri wa DiDi" inakabiliwa na kashfa ya kutumia vibaya teknolojia ya Big Data.
Wanamtandao wengi wamefanya majaribio baada ya kuibuka kwa kashfa hiyo, na kugundua kuwa "wakati mmoja, sehemu moja ya kuanzia na kumalizia safari, wateja wawili tofauti wanakadiriwa kulipa nauli tofauti wakiita teksi kwenye app hii." Kwa mfano, Li anatumia app ya DiDi kuita teksi mara kwa mara anaporudi nyumbani kutoka kazini, na yeye alimwita mwenzake ambaye hajawahi kufutumia njia hii anayotumia Li kumsaidia kwenye uchunguzi huo, matokeo yake yaliwashangaza watu. Mbali na coupon, Li anayetumia njia hii mara kwa mara alikadiriwa kulipa Yuan nne zaidi kuliko mwenzake!
Big Data ni neno linalotajwa sana katika zama za leo, na karibu kila kampuni ya mtandao inatumia teknolojia hii kufanya uchunguzi kwa wateja wao, kujua undani wa "picha ya mteja" na kuamua kupanga bei kama binadamu kwa mujibu wa kiwango chao na hisia zao juu ya bei kwa mujibu wa app zao.
Kwa mujibu wa uwezo wa mteja, kadiri mteja anavyokuwa tegemezi sana kwa app hiyo na kuwa na imani nayo, ndivyo hisia zake kuhusu bei zinavyopungua, na mteja kama huyo ndio chanzo kikuu cha mapato kwa watumiaji wa app hizo. Kitendo hicho kinatafsiriwa kuwa ni "Big Data kuwaua wateja wa kawaida"
Wanamtandao wanasema kitendo hicho sio tu kiko kwenye app za kuita teksi, pia kiko kwenye app na tovuti za kununua tiketi za ndege, kuoda hoteli, kununua tiketi za filamu na kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Lakini ofisa mkuu wa teknolojia wa Didi Zhang Bo amesema DiDi haijawahi na daima haitatumia mbinu hii ya eti "Big Data kuwaua wateja wa kawaida". App hii hairuhusu ubaguzi wa bei, na nauli haitakuwa tofauti kutokana na watu tofauti au chapa tofauti za simu za mkononi wanazotumia.
Hata hivyo, kashfa kama hiyo pia inaikabili kampuni nyingine maarufu ya mtandao wa kijamii ya Facebook. Habari zinasema kampuni ya uchambuzi wa matangazo ya kisiasa Cambridge Analytica imetumia taarifa za watumiaji zaidi ya milioni 50 wa Facebook bila idhini ya Facebook. Hivi karibuni, kampuni ya Facebook ilitangaza matangazo kwenye magazeti sita ya Uingereza na matatu ya Marekani na kuomba radhi kutokana na kashfa hiyo. Ofisa mkuu mtendaji wa Facebook Bw. Mark Zuckerberg alisisitiza kuwa Facebook imezuia app nyingine kutumia taarifa za watumiaji wake kupitia Facebook, na kusema kampuni hiyo imefanya hivyo tangu watu walipoanza kusajiriwa kwenye FB. Amesema "hiki ni kitendo cha kukiuka uaminifu, sikufanya juhudi zaidi wakati ule, naahidi kukufanya vizuri zaidi."
Kinachofuatiliwa ni kuwa kabla ya vyombo mbalimbali vya habari kuitangaza kashfa hiyo, Zuckerberg hakuonyesha hata kidogo nia ya kuomba radhi, na alilazimika kuomba radhi alipohojiwa na CNN.
Lakini watumiaji wengi wa Facebook wanapuuza kuomba radhi kwake na kufanya kampeni ya #deleteFacebook kwenye FB, na wengi wameanza kujitoa kwenye FB akiwemo afisa mkuu mtendaji wa Tesla bilionea Elon Musk.
Habari zinasema Facebook inauza takwimu za watejai wake kwa mwenzi wake kampuni ya uchambuzi ya Cambridge Analytica kwa mujibu wa kipengele cha huduma. Cambridge Analytica iliwahi kuwa timu ya uchambuzi wa takwimu iliyomsaidia rais Donald Trump kwenye uchaguzi wake mwaka 2016.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |