• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BETEL NUT YAKUZA UCHUMI WA WANNING

    (GMT+08:00) 2018-04-17 09:19:55

    Na Trix Ingado

    Kwa wengi katita maeneo tofauti ya dunia, Betel nut ni kitu ambacho hawajawahi kukiskia wala kuonja. Licha ya hayo, njugu hii imekuwa nguzo ya uchumi wa mji wa Wanning mkoani Hainan.

    Njugu hii ina ladha chachu ambayo pengine ndio sababau inapendwa sana na watu kama vile madereva wa magari kwani inaweza kuwasaidia kuwa makini barabarani. Ni ladha ambayo huweza kuwa ngumu kustahimili kwa mtu ambaye hajaizoea lakini inapendwa sana na wenyeji wa eneo hili kwani miti ya njugu hii inayojulikana kama 'Betel Palm inakuwa kwa wengi.

    Kwa sababu ya umaarufu wa njugu kampuni ya Kouweiwang Development Company ilianzishwa mwakani elfu mbili na kumi. Kampuni hii imesaidia katika kusambaza umaarufu wa betel nut.

    Kuna viwanda viwili vya kutayarisha Betel Nut jijini Wanning. Ya kwanza ikiwa Houan iliyoko katika mji wa Houan. Kiwanda hiki kiko katika kipande cha ardhi cha ukubwa wa hektari sita nukta tisa na ina thamani ya milioni mia moja thelathini.

    Kiwanda hiki kimewapa kazi wenyeji elfu moja sabini na saba. Kiwanda cha pili ambacho bado kinajengwa, ni cha Dongao na kiko kwenye ardhi ya ukubwa wa hektari kumi na tano nukta nane iliyona dhamana ya RMB mia mbili na moja.

    Viwanda hivi huisafisha kisha huongeza ladha tofauti na kuiweka katika karatasi nyekundu zitakazo hakikisha zitauzwa katika maduka kote China zikiwa safi.

    Mwakani elfu mbili na saba, idadi ya wafanyikazi katika kiwanda hiki walikuwa elfu moja tisini na mbili, lengo la wakuu wa kiwanda hiki wanatarajia kuwaajiri angalau wafanyakazi elfu tatu inapokamilika. Hii itasaidia kuleta ajira kwa takriban watu elfu mbili mia sita tisini na tisa na kupunguza umaskini kati ya wenyeji.

    Kando na hayo kampuni hii imeweza kuwaajiri wenyeji mia nne wanaoishi chini ya kiwango halali cha umaskini na thelathini na moja wanaoishi na ulemavu.

    Ili kuinua jamii ya Huoan , kampuni hii hununua njugu kutoka kwa wenyeji. Tangu mwaka jana mwezi wa Aprili , kiwanda hiki kimeweza kununua tani zaidi ya milioni saba nukta tano na kutoa malipo zaidi ya milioni mia sita tisini na tisa kwa wakulima wa Huoana.

    Kati ya wakulima hao, mia moja kumi na wawili walipata hela kutokana na kukaanga njugu hizi huku wengine elfu arobaini na nne kutokana na mazao yao ya shamba.

    Juhudi za kampuni hii, mbali na faida za kibiashara pia zinaambatana na malengo ya serikali kuu ya Rais Xi Jinping ya kuondoa umasikini nchini China.

    Mwaka huu wa 2018, wanatarajia kupata mazao kiasi cha tani elfu saba , mia moja katika paketi milioni kumi na tisa itakayo kuwa na dhamana ya bilioni moja nukta moja.

    Njugu hii inamanufaa tofauti kwa afya ya binadamu, kwa mfano, kupitisha chakula tumboni, kuongeza mate mdomoni and kusaidia kuwa makini.

    Mmea wa Beatle Palm, unapatiakana pia nchini India , Japan, Sri Lanka, East Indies, Phillipines Bangladesh, na maeneo fulani ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako