• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi masuala ya Afrika azungumzia maandalizi ya FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-05-02 08:49:40

    Na Majaliwa Christopher

    Maandalizi ya mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika mwezi Septemba, jijini Beijing, unaendelea vizuri.

    Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Dai Bing wakati akifanya mazungumzo na waandishi wa habari kutoka Afrika walioko nchina China katika programu maalum ya mafunzo.

    Mkutano huo utakaojikita pamoja na mambo mengine, katika masuala ya biashara, teknolojia, diplomasia, kilimo, utamuduni na uendelezaji wa rasilimali watu, utaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha ushirikiano kati ya China na Afrika.

    "Mapema mwezi wa tisa, mkutano wa FOCAC utafanyika jijini Beijing. Tunafaya kazi kubwa kuhakikisha unakuwa wa mafanikio wa hali ya juu, maandilizi yapo katika hatua nzuri," alisema.

    Alisema kuwa wakati huohuo China inashirikiana na nchi za Afrika katika kutekeleza maazimio mbalimbali waliyofikia katikia mkutano uliyofanyika jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini, mwaka 2015.

    Katika mkutano huo wa Johannesburg ulioongozwa na Rais Xi Jinping wa China kwa kushirikiana na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, China iliahidi kutoa jumla ya dola bilioni 60 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo barani Afrika.

    Sehemu ya fedha hizo, kwa mujibu wa Bw. Dai ni kwa ajili ya mikopo yenye masharti nafuu na zingine zikiwa ni msaada yasiyokuwa na masharti na kuwa ahadi hiyo imeshatekelezwa kwa kiasi kikubwa.

    Kuhusu uwekezaji barani Afrika, Bw. Dai alibainisha kuwa hadi kufikia mwaka 2015, uwekezaji wa China Afrika ulifika takribani dola za Kimarekani bilioni 100 huku kampuni za China zikiwa ni zaidi ya 3,000.

    "Afrika inategemewa kuendelea kukuwa huku uchumi wake ukizidi kuimarika, nina uhakika wawekezaji wengi kutoka China wataendelea kumiminika barani humo," alisema.

    Kwa upande mwingine, Bw. Dai alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika utaendelea kuwa wa kunufaishana bila masharti yoyote ya kisiasa.

    "Mwanzoni, Afrika haikuwa na chaguo. Kwa sasa bara hilo lina nafasi ya kuchagua namna ya kufanya mambo yake, kuchagua upande utakaolinufaisha zaid," aliongeza.

    Bw. Dai alisema kuwa Afrika na China ambazo kwa ujumla zina idadi karibia theluthi tatu ya dunia nzima, zikisimama pamoja na kushirikiana katika maendeleo endelevu, zina uwezo wa kubadilisha maendeleo ya dunia.

    "Sauti ya China haiwezi kusikika. Sauti ya Afrika haiwezi kusikika pia. Tukiunganisha sauti zetu kwa pamoja tutasikika," mkurungenzi Dai alisema.

    Aliongeza kuwa kama ambavyo ushirikiano wa pande zote mbili zimejengwa katika misingi ya urafiki na undugu, wataendelea kusisitiza umuhimu wa kukaa mezani kushughulikia changamoto yoyote inayoweza kuathiri mahusiano yao.

    China pia imesisitiza kuwa wataendelea kuweka kipaumbele katika masuala ya maendeleo na kamwe hawataingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika kwani wanaheshimu uhuru wa kila nchi.

    Bw. Dai aliongeza kuwa nchi yake ina dhamira ya dhati kusaidia juhudi za kuleta amani na usalama Afrika ili kila sehemu ya bara hilo liwe sehemu bora na salama kuishi.

    "Tumekuwa mstari wa mbele katika kutoa maaskari wetu kushiriki ulinzi wa amani barani Afrika, hadi muda huu tunaongea Wachina watatu wameshapoteza maisha barani humo wakiwa katika majukumu ya kulinda amani," alisema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako