Naibu wa Rais wa Uchina Bw. Wang Qishan hii leo alisema kwamba China haiwezi kujiendeleza bila ushirikiano na nchi zingine.
Alitamka maneno haya katika ukumbi wa Ushirikiano kati ya serikali za ugatuzi za China na za nchi tofauti barani Afrika.
Ni katika hotuba yake hii leo ambapo alisisitiza kwamba China ipo tayari kwa vyovyote vile kutumia maendeleo yake kuisaidia Afrika kuendelea.
Ushirikiano kati ya China na Afrika umebainika kwa njia tofauti katika miaka michache iliyopita ikiwemo mafunzo ya kitaalamu, masomo ya bure , ushirikiano kati ya serikali za mikoa ya China na mikoa ya nchi tofauti Africa na biashara kati ya eneo hizi mbili, alisema Bw. Wang.
Licha ya kuwepo kwa ushirikiano huu serikali ya China bado inatarajia kuendelea na kuweka wazi ujuzi wake upande wa maendeleo yanayowafaidi wananchi.
Kando na hayo Naibu wa Rais aliwarai viongozi wa nchi za Afrika kukaza kamba katika maswala ya maendeleo na kuweka mipango kabambe itakayo wafaidi Waafirika sio kwa kuiga China bali kwa kuzingatia mahitaji ya raia wao wanaohitaji faida za maendeleo ya uchumi.
Kwa upande wake China itaendelea kuwahimiza raia wake kujishirikisha katika uwekezaji barani Afrika ila tu bishara hizo zisiwe biashara zinazodhuru mazingira safi ya bara Afrika.
Matamshi ya Bw. Wang yaliungwa mkono na Waziri mkuu wa Niger Bw. Rafini Brigi aloyeisifu serikali ya China kwa juhudi zake za kuleta maendeleo kwa dunia kwa njia ya amani huku akinukuu maatamshi ya aliyekuwa kiongozi wa Ufaransa Napoleon Bonapate "Dunia itatikisika China itakapoamka."
Niger na China ni nchi ambazo zimeshirikiana kwa maeneo tofauti kama vile miradi ya maji safi ya kunywa, kilimo, afya ya umma, nguvu za umeme, sekta ya usafiri , usalama na kadhalika.
Waziri huyo Mkuu aliweka wazi kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili ni wa faida kwa maeneo yote mbili huku akifichua kuwa kuna miradi nyingi nyingine iliyo jikoni.
Brigi hata hivyo alisisitiza kwamba ili kufuzu katika juhudi za kuondoa umaskini barani Afrika na China ni muhimu kwa viongozi wa maeneo yote mbili kuyapa mahitaji ya wananchi wa kawaida kipaumbele.
Kupitia uongozi wa rais Mahamadou Issoufu, serikali ya Niger kwa sasa inatumia mpango wa kuondoa umaskini maarufu kama renascence mradi unaoambatana na mada ya mkutano wa ushirikiano kati ya serikali gatuzi za nchi tofauti za bara Afrika na China.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania pia alitoa wosioa wake katika sherehe ya kufunguliwa kwa mkutano ambapo aliweka wazi kuwa ili Afrika kutia fora katika maswala ya uchumi , biashara na maendeleo, ni muhimu kutokuwepo na hatari ya kudhalilishwa na kutumiwa vibaya nan chi zilizoendelea.
Ni kwa sababu hii, alisema , nchi nyingi barani zimeamua kujishirikisha na China nchi ambayo iliiunga Tanzania mkono kimaendeleo haswa katika nyakati ambazo China yenyewe haikuwa imeendelea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |