Na Trix Ingado
Tamasha Dragon Boat, al maarufu Duanwu Festival ni tamasha ya kitamaduni nchini China. Tamasha hii husheherekewa kila mwezi wa tano tarehe vtano kulingana na kalenda ya Kichina. Chanzo cha tamasha hii muhimu ni kumbukumbu ya kifo chawaziri na mshairi Qu Yuan aliyeishi kati ya miaka ya 340 – 278 BC.
Mshairi huyo anakumbukwa kwa umaarufu wake wa utenzi na kifo chake kilicho wahuzunisha wengi. Inasemekana Qu Yuan alijitosa mtoni Miluo pindi alipogundua kuwa aliyekuwa kiongozi wa eneo la Qin alikuwa amechukua mamlaka katika la eneo la Chu alikotorokea baada kutuhumiwa kuwa msaliti alipoishi Qin.
Jambo hili liliwasikitisha wakaazi kiasi cha wao kumfuata majini katika mashua ilikumuokoa au angalau kuupata mwili wake. Licha ya juhudi zao, wenyeji wa mji wa Chu hawakuweza kumuokoa. Hivyo basi wakaamua kuchukua mchele na kuutupa majini ili samaki wale mchele badala ya mwili wake.
Masikitiko yao yalipelekea kuanzishwa kwa tamasha hii kama kumbukumbu ya umahiri wake katika uongozi na ushairi. Mapishano ya mashua ni mojawapo ya shughuli zinazofanyika katika siku hii kuu kila mwaka. Wali pia hupikwa katika majani spesheli na mlo huu huliwa siku hii.
Mvinyo halisi wa aina ya realgar hutayarishwa na kubugiwa na wenyeji kote nchini China. Mvinyo huu pia unatengenezwa kutokana na mmea wa Realgar ambao hutumiwa pia kufukuza mb una ni tiba ya sumu mwilini. Pia, wenyeji hushona kamba spesheli zinazoaminiwa kuleta afya nzuri na kulinda wanaozifaa kutokana na mapepo mabaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |