• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na utamaduni wa unywaji chai

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:15:44

    Na Christopher Oswero

    KWA nchi nyingi duniani, chai ni kinywaji tu na mara nyingi hunywewa wakati wa asbuhi kama sehemu ya kifungua kinywa.

    Mbali na kutengenezwa na kunywewa asbuhi kama sehemu ya kifungua kinywa, wengine hupenda kunywa chai ili kudhibiti hali ya baridi.

    Lakini, nchini China, hali ni tofauti. Chai ni sehemu ya utamaduni. Hunywewa asbuhi, mchana, jioni na usiku. Kwa kifupi kila wakati China, ni wakati wa Chai tena ni chai isiyotiwa sukari!

    Mgeni yeyote, wakati wowote anapotembelea familia yoyote nchini China, baada ya salamu, kifuatacho ni chai tena bila hata kuulizwa na utaongezwa bila kuulizwa. Huu ni utamaduni wao. Wanaupenda na wanaudumisha.

    Pamoja na kuchangamsha mwili kwa ladha ya kipekee, Wachina wanaamini kuwa chai ina faida nyingi kiafya, kiasi cha kuifanya kuwa kinywaji cha muhimu na lazima.

    Historia inaonyesha kuwa chai kwa miaka ya nyuma ilikiwa inatumika kwa matamabiko mbalimbali nchini China na majani ya chai yalikuwa yakiliwa kama mboga au dawa kwa ajili ya kutibu maradhi mbalimbali.

    Lakini kwa sasa, hali imekuwa tofauti. Unywaji chai nchini China imekuwa ni utamaduni na sehemu ya maisha ya kila siku.

    Serikali nchini humo imeenda mbali zaidi na kujenga maeneo maalumu, kimsingi, kwa ajili ya kuhakikisha utamaduni huu unadumishwa na kuendelezwa.

    Maeneo haya kwa ajili ya kudumisha utamaduni wa unywaji chai, kwa mujibu wa takwimu zilizopo, yako zaidi ya 25,000 na yameajiri mamilioni ya watu.

    Lakini pia kuna mambo mengi zaidi yanaendelea katika maeneo haya zaidi ya kunywa chai--kuna maonyesho mbalimbali ya kiutamaduni.

    Jijini Beijing, mji mkuu wa China, jiji lenye wakazi wapato milioni 22, Laoshe Teahouse, ni moja ya maeneo maarufu ambapo chai ya asili inapikwa na kuuzwa.

    Watu wengu hujaa eneo hili, ambapo wapita njia pia wanaweza kusimama na kujinunulia chai na kunywa nje ya jengo wakati wowote na siku yoyote--iwe asbuhi, mchana au jioni.

    Kwa ndani, imepambwa kwa maua mazuri ya kuvutia, viti vimepangwa kwa ustadi mkubwa huku wahudumu wazoefu na wanadhifu wakiwa tayari kila wakati kupokea na kuwahudumia wageni.

    Bw. Jiao Yin, mmoja wa maafisa wa juu katika jengo hili anasema pamoja na kutoa huduma ya chai ya asili, lakini eneo hilo pia kwa sasa imekuwa kivutio kikuu cha watalii jijini Beijing.

    Anasema Laoshe Teahouse, kutokana na upekee wake, ni moja ya maeneo muhimu kwa ajili ya mapumziko na burudani huku ikiwa ni kielelezo na mfano sahihi wa utamaduni wa nchi na maisha ya wenyeji wa China.

    Anaongeza kuwa, tafauti na kutembelewa na watu wengi wa kawaida kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi mbalimbali kutoka mataifa mbambali pia wamewahi kutembelea eneo hilo na kufurahia huduma wanazotoa.

    Kwa mfano, mwaka 1994, Bw. George Bush, Rais wa zamani wa Marekani alitembelea aneo hilo, huku mwaka huu, 2018, Waziri Mkuu wa Uholanzi Bw. Mark Rutte na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres wametembelea Laoshe Teahouse.

    Kwa mujibu wa Bw. Jiao, kwa siku wastani wa bakuli 1,000 za chai zinauzwa kwa huku akibainisha kuwa mwaka 2008 wakati wa Olimpiki mauzo kwa siku yalikuwa yakifika hadi bakuli 3,000 kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako