• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utangamano wa Waafrika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:47:08

    Na Trix Ingado

    Huku kongamano la FOCAC likikaribia, hatuna budi kutafakari uhusiano kati ya China na bara la Afrika.

    Kama tunavyo jua bara la Afrika linajitahidi kuendelea kiuchumi na ni kwa sababu hii , nchi tofauti zimechagua kushirikiana na China katika miradi nyingi zitakazosaidia jitihada hizo.

    Katika kongamano la mwaka wa 2015 kule Johannesburg, Afrika Kusini, China ilipendekeza miradi na sera zitakazo faidi pande zote za uhusiano huu.

    Kufuatia uhusiano huu, juhudi za biashara, na ushirikiano katika sekta za elimu, afya, mazingira na kadhalika zimepelekea kusafiri kwa Wachina wengi kuenda Afrika na pia Wafrika wengi kuja China.

    Kwa sababu ya tofauti za mila na desturi, ni vyema kuelewa jinsi ambavyo watu kutoka bara la Afrika wameweza kuishi na kutangamana na Wachina.

    Jamii ya Waafrika China haswa mjini Beijing ni kubwa mno , unaweza kuigawanya katika vikundi vitatu, wanafunzi, wanafanyakazi na wanyifibiashara na wanadiplomasia.

    Kulingana na takwimu za shirika la kimataifa la UNESCO, kufikia mwaka wa 2015 idadi ya wanafunzi wanaokuja China kutafuta masomo ya juu imeongezeka kwa mara ishirini na sita.

    Hii inaonyesha kwa muonekano wa China kwa dunia na haswa kwa Waafrika umepata kubadilika , wengi wanasema hii ni kwa sababu ya sera ya kufunguka inayotekelezwa na serikali ya China.

    Miaka Kumi China

    Mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya CRI Pili Mwinyi Khamis ni mfano mzur i wa utangamano kati ya Wachina na Waafrika . Ameishi Beijing kwa miaka kumi. Kwake yeye, sura ya China inaendelea kubadilika.

    Hapo zamani ilikuwa inakisiwa kuwa nchi ambayo haija endelea kwa hivyo wengi hawakuwa na hamu ya kuja China kujitafutia riziki.

    Bi Khamis anasema, 'Lakini jinsi mambo yanavyozidi kubadilika , watu wanarudi nyumbani ya kuwahadithia wenzao kuhusi hali ilivyo siku hizi . Wengi wana sema , 'Ah siku hizi China ni Ulaya!'

    Taarifa hii imeenea kwa mda na inawapa wengi ujasiri wa kutaka kujitafutia riziki China.Yeye ameweza kuishi salama Beijing kwa miaka hii pamoja na mumewe na mwanawe.

    Miaka Tano China

    Katika kongamakno la FOCAC la 2015, China ilijitolea kusaidia vijana wa Afrika kupata masomo kupitia miradi ya masomo ya bure. JUhudi hii inatarajiwa kusadia katika kuondoa janga la umaskini , kwani jamii elimu na taaluma ndio vigezo muhimu vinavyohakikisha uwezo wa kujikimu maishani.

    Robert Ochola ni mmojawapo wa walionufaika kutokana na miradi hii. Anaeleza jinsi alikuwa mfanyakazi wa serikali katika wizara ya kilimo alipopata udhamini wa masomo.

    'Niliona tangazo kwenye gazeti na nikaamua kulichngamkia. Sikutarajia kuchaguliwa lakini kwa bahati nzuri nikapata ile fursa. Kwa hivyo mwakani 2012 nilikafunganya vyangu na kuhamia Beijing' Kasema Bw. Ochola.

    Mda si mrefu akateuliwa kuwa mwenyakiti wa chama cha wanafunzi Wakenya Beijing. Ni kupitia cheo hiki ambapo alijulishwa na ubalozi wa Kenya China kuhusu fursa ya kujiunga na kampuni ya StarTimes.Amekuwa akifanya kazi pale tangu 2012 hadi leo.

    Jukumu lake kuu lilikuwa kutafsiri na kutia sauti ya kiume katika mazungumzo ya vibonzo na filamu za kuigiza.

    'Nilifanya kazi hiyo hadi nilipokamilisha masomo yangu. Hapo ndipo StarTimes walipopendekeza nijiunge kama mwajiriwa. Nilirudi Kenya kwa mwaka moja na baadaye nikarudi Beijing kuanza kazi rasmi.' Kasema Ochola.

    Anasema kwamba kuna wengi nchini kama yeye ambao wanaishi na kujipati riziki. Robert anasema kwamba ni muhimu kwa wote wanaotafuta fursa China kujishirikisha na kampuni zilizonamisingi dhabiti.

    Pia anasema ni muhimu kujishirikisha na biashara halali na kuwa na stakabadhi zinazohitajika ilikuishi China kihalali na kwa amani.

    Leo, Bw. Ochola yupo katika fani ya kutia sauti licha ya kuwa na masomo katika ukulima, anatumahi huileta familia yake kujiunga naye Beijing, pindi stakabadhi zao zitakapokuwa tayari.

    Mwaka mmoja China

    Edwin Thuo Mwai kutoka Kenya pia alikuja Beijing mwaka jana kwa sababu ya masomo. Yuanieleza kwamba alipowasili mwezi Machi mwaka jana, ilikuwa vigumu kwake kuyazoea maisha mapya kwa sababu ya ya karidi kali.

    Lakini mda si mda alizoea maisha na kuendelea na kosi yake ya civil engineering bila tatizo. Yuasema kwamba anamatumahi ya kurudi nyumbani na kufanya kazi huko pindi tu atakapomaliza masomo yake chuoni.

    Bw. Mwai ni mmoja kati ya wanafunzi wapatao sitini wanaosoma katika chuo cha Beijing Jiaotong University.

    Mwai anapendezwa sana na mandhari ya Beijing na anapokuwa na mda yeye hupenda kuzuru mji wa Beijing kwenye baiskeli yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako