Jambo moja lisiloweza kupingwa ni bidii ya Wachina kudumisha historia,kwa kuhifadhi majengo yao vifaa, hadithi na hata ushairi wao. Lolote lililonaumuhimu wa kihistoria utalipata leo likiwa limetunzwa licha ya kuwa na asili ya jadi.
Unapozuru Shanghai taswira hii ya mambo yalivyo kuwa enzi za kikoloni ipo, muhimu zaidi, historia ya kisiasa ya China tunavyo ijua leo ipo mjini Shanghai kwani chama tawala cha CPC kina asili yake Shanghai. Chama tawala cha CPC kilianzishwa katika jumba moja katika kitongoji cha Xintiandi, nambari 76 -78 barabara ya Xingye.
Ili kuelimisha vizazi vipya kuhusu historia hii, jumba hilo la aina ya shikumen limewekwa wazi kwa wote walionahaja ya kujua yaliyojiri. Hapa ndipo unapoweza kuhadithiwa jinsi mnamo tarehe ishirini na moja Julai mwaka wa elfu moja mia tisa ishirini na moja wajumbe kumi na tatu walikutana kwa ajili ya kuanzisha chama hicho licha ya changa moto si haba. Cha kufana ni kwamba tangu jengo hili lilioekwa katika ulinzi wa serikali mwakai elfu moja mia tisa hamsini na mbili hali ileile. Baraza la kitaifa liliiratibisha kuwa makavazi ya kihistoria mwakani elfu moja mia tisa sitini na moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |