• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FOCAC 2018 NA MATARAJIO YAKE

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:46:33

    Na Trix Ingado

    Mwakani 2015 kongamano kuu la Forum for China Africa Corporation yaani FOCAC lilifanyika mjini Johannesburg Africa Kusini. Sababu kubwa ya mkutano huu ilikuapanga mbinu ambazo China na nchi mbalimali barani Afrika zingeweza kushirikiana katika maswala ya maendeleo.

    Kwa sababu ya mahitaji mazito ya nchi husika, mipango na malengo makubwa yaliyoratibishwa ikawa dhahirii kwamba mwelekeo wa kuboresha pande zote utakuwa bora. Ni kwa moyo huwo ambapo dola bilioni sitini zilitolewa na Uchina kwa minajili ya kufululiza mipango.

    Hela hizo ziligawanyika hivi, bilioni tano kwa kwa biashara huria na mikopo bila riba, bilioni thealathini na tano kwa mikopo, bilioni tano kwa hazina ya maendeleo ya China-Afrika pamoja na maendeleo ya biashara ndogo na bilioni kumi kwa ushirikiano katika uzalishaji.

    Katika miaka kadhaa zilizofwata, China na nchi teule zilijishughulisha katika juhudi na miradi katika nyanja na sekta limbali kama vile afya, elimu, miundombinu, biashara, kilimo na kadhalika. Huku Beijing ikiwa katika pilkapilka za kujiandaa kwa mkutano ujao wa FOCAC inatarajiwa kwamba viongozi watakaohudhuria, wengi wao marais na mawaziri, inatarajiwa kwamba ajenda kubwa itakuwa kutathmini juhudi zimefika umbali gani. Kisha maamuzi yatafanywa yatakayo dumisha juhudi hizi.

    Lengo moja kuu ni katika kutengeneza ajira kwa kuondoa umaskini. Hii inalengwa na kupitia hela zilizotengwa ilikujenga biashara ndogondogo. Pia kuna ushirikiano wa biashara ambani zipo kampuni za Kichina zinazoanzishwa barani zinazonufaisha jamii kupitia ajira kwa vijana. Vijana hawa wanapopata mbinu za kujikima maishani jamii kwa ujumla inanufaika, vilevilekampuni za Kichina zinapata soko za kuuza bidhaa. Kampuni hizi pia zimeweza kuwahakikishia Wachina ajira kwani wataalamu wanaohitajika wameweza kuhamia Afrika ilikuendeleza na kustawisha biashara hizi. Inasemekana wenye kampuni zinazolenga.

    Soko za Afrika wanaona afadhali wajenge viwanda barani Afrika iliwakaribie masoko yao. Kwa mtazamo huu wa ushirikiano, inatarajiwa kwamba kupita kufanya kazi kwa karibu wataweza kufunzana vitu mbalimbali kwa mfano watengeneza simu ya infinix wamekuwa na kiwanda nchini Ethiopia kwa miaka kadhaa sasa. Hii imewawezesha kukaribia wanunuzi wa simu hiyo ya Kichina inayouzwa Afrika pekee.

    Licha kuwepo kwa juhudi mpya za kukaribiana haswa kati ya wanadiplomasia, wanasiasa na wafanyibiashara kutoka pande zote mbili, ni muhimu kufahamu kwamba biashara kati ya bara Afrika na China sio jambo geni.

    Historia inatueleza kwamba zaidi ya miaka mia tano iliyopita Wachina walizoea kusafiri kwa meli hadi Afrika mashariki kwa nia kufanya biashara. Walikuja na bidhaa za Kichina na kuondoka na bidhaa za Kiafrika.

    Hii ni ishara kwamba ushirikiano huu unawezajengeka ila ni muhimu kwa wadau kuwa makini na kuzingatia sheria, matakwa ya pande zote, udumishaji wa mazingira mazuri na kandarasi zilizotiwa sahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako