Na Theopista Nsanzugwanko
CHINA imesema iko tayari kuanzisha mfuko wa maendeleo na mikopo kwa Afrika huku ikiandaa maeneo ya ujenzi wa viwanda katika ukanda huo.
Nchi hiyo ya pili wa uchumi duniani imesema lengo ni kusaidia nchi hizo kukamilisha ndoto ya ujenzi wa viwanda kwa maendeleo endelevu.
Aidha, Balozi wa Taasisi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Zhou Yuxiao amezitaka nchi za Afrika kutarajia miradi zaidi ya ushirikiano kwa Tanzania na Afrika baada ya mkutano wa pili wa FOCAC utakaofanyika Septemba mwaka huu.
Mwakilishi wa biashara na uchumi wa China nchini, Lin Zhiyong alibainisha hayo hivi karibuni wakati wa mkutano baina ya Chama cha Kimomunisti cha china (CPC) na Vyama vya siasa Afrika.
Anasema China iko tayari kuwekeza maeneo mbalimbali kwa kuzingatia uchumi itaandaa maeneo kwa ajili ya viwand akatika nchi za Tanzania,Kenya , Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Misri na mengine mengi.
Anasema ushirikiano kati ya Afrika na China kwa sasa kumekuwa na mtandao mpya wa ushirikiano baina ya Afrika na China (FOCAC) uliosaidia uwekezaji wa kibiashara kufikia dola bilioni 107 huku uwekezaji ukiwa dola bilioni 43.
"Kwa sasa uwekezaji katika nchi za Afrika umekuwa ukipungua kutokana na nchi nyingi kuwa na migogoro ya vita vya wenyewe kwa wenyewe au migogoro mingine ni vema kukaa na kuangalia namna ya kukabiliana na migogoro hiyo," anasema
Zhiyong anasema maeneo hayo ya viwanda yatasaidia kufikia maendeleo endelevu na kusaidia nchi za Afrika kufanya baishara na China na kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi na mapato ya mtu mmoja mmoja.
Alisema kila mwaka nchi imekuwa ikisaidia kutoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa nchi za Afrika na misaada mbalimbali hivyo alihaidi kuendele akutoa misaada ya Nyanja mbalimbali bila masharti.
Zhiyong anasema nchi nyingi zilizoendelea zinafunga milango kwa nchi za Afrika kufanya baishra lakini waoa wamefungua milango hiyo kusaidia maendeleo Afrika na kutaka kuongeza bidhaa kuuza nje ya nchi.
Balozi Yuxiao Anasema katika mkutano wa Ushirikiano baina ya pande hizo mbili,utakaofanyika Septemba mwaka huu wataweka mikakati na hatua mpya kuendeleza Afrika kwa kutumia fursa zilizopo.
Anasema Tanzania ni sehemu muhimu katika Afrika kutokana na historia ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili kuanzia nyakati za kutafuta uhuru kwa nchi za Afrika,China ilipojenga reli kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Anasema kwa wakati ule hawakuwa matajiri, bali ni katika kudumisha urafiki na undugu baina ya pande hizo mbili.
Anasema hata Rais wa China aliposhika madaraka, nchi ya kwanza kutembea Afrika ilikuwa Tanzania na sasa mkutano mkubwa baina ya China na vyama vya siasa Afrika umefanyika Tanzania.
Anazungumzia mataraji ya Tanzania na Afrika katika mkutano wa FOCAC, anabainisha kuwa tangu kuanza kwa Jukwaa hilo kumekuwa na ushirikiano mkubwa katika miradi mingi ya maendeleo Afrika ambayo mingine imeanza na ipo inayoendelea kutekezwa.
Anasema anatarajia kuwa miradi mingi zaidi katika miaka ijayo kwa Tanzania na nchi nyingine Afrika.
"Katika wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kiutawala na masuala ya ndnai kukaa sawa ,natarajia miradi mingi itafuata kwa ushirikiano na China na nchi nyingine za Afrika," anasema.
Anahaidi katika kuhakikisha ushirikiano baina ya China na nchi za Afrika unaimarika zaidi kama balozi wa masuala hayo nchini China.
Inaelezwa kuwa biashara baina ya China na Afrika umefikia dola za Marekani bilioni 99.84 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.3 kila mwaka.
Wizara ya biashara China inaeleza kuwa ,Juni pekee ,biashara baina ya China na Afrika imefikia dola za Marekani bilioni 16.82 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 kutoka mwaka uliopita.
Uuzaji wa biashara Afrika unaongezeka kwa asilimia nane kila mwaka kwa dola zamarekani bilioni 9.3 huku uingizaji bidhaa ni bilioni 7.52 ikiwa ni ongezeko la asilimia 24.4 kila mwaka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |