• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FOCAC kuhusianisha Ukanda Mmoja, Njia Moja na agenda za AU, UN

    (GMT+08:00) 2018-08-23 16:02:11

    Oswero, Beijing

    Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, utakaofanyika kati ya Septemba 3 na 4 unategemewa kuhusianisha malengo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Maendeo Endelevu na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

    Wakati Ukanda Mmoja, Njia Moja ukilenga kuunganisha bara la Asia, Afrika na Ulaya kwa njia ya miundombinu mbalimbali, agenda za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zinalenga kutatua changamoto mbalimbali za kimandeleo barani Afrika na duniani kwa ujumla.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Bw. Wang Yi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Beijing, alisema kuwa dhima ya mkutano huo pia utaegemea katika malengo ya maendeleo ya kila nchi ya bara la Afrika.

    Nchi 53 kutoka bara la Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China zitahudhuria mkutano huo wa siku mbili huku Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Bw. António Manuel de Oliveira Guterres akitegemewa kuhudhuria kama mgeni mwalikwa.

    Kwa mujibu wa waziri Wang, nchi zote za Afrika zitakazohudhuria mkutano huo pamoja na China zitapitisha kwa pamoja mambo mbalimbali ya ushirikiano katika nyanja mbaimbali ikiwemo miundombinu, kilimo, afya, namna ya kupambana na umaskini, biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama.

    Alisema kuwa mkutano huo utakaofungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya China na Afrika utakuwa kichocheo cha kuimarika kwa mahusiano kati ya pande hizo mbili zenye malengo ya kunufaishana.

    Aliongeza kuwa tangia kuanzishwa kwake miaka 18 iliyopita, Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, umekuwa chombo muhimu cha ushirikiano chenye muelekeo wa kuimarisha mapambano dhidi ya changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

    Bw. Wang alisema kuwa jukwaa hilo litakuwa pia chachu ya utekelezaji wa miradi chini ya Ukanda Mmoa, Njia Moja na makubaliano mbalimbali yatakayosainiwa kati ya pande hizo mbili yatatumika kama hadidu za rejea na muongozo kwa miaka mingine mitatu ijayo.

    "Kwa miaka 18 iiyopita tangu kuanzishwa kwake, jukwaa la FOCAC limekuwa kichocheo muhimu cha maendeleo katika nyanja mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hasa baada ya mkutano wa Johannesburg wa 2015," alisema waziri Wang.

    Aliongeza kuwa; "Mipango mbalimbali ya maendeleo iliyotangazwa kwenye mkutano wa 2015 wa FOCAC umezidi kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika na kukubalika miongoni mwa watu wa bara la Afrika na mataifa mengine nje ya bara hilo".

    Katika mkutano unaokuja, Bw. Wang alisema Afrika na China zitafikia malengo yake kwa kupitia kwa mdahalo wa pamoja wa kiundugu na kirafiki na wa kuheshimu mchango wa kila nchi mwanachama.

    Alisema pia kuwa Rais wa China atatumia mkutano huo kutangaza hatua mpya za kimandeleo na ahadi za nchi hiyo kwa bara la afrika zitakazokuwa dira na alama zitakazotoa muelekeo wa ushirikiano katika miaka ijayo.

    Katika mkutano uliopita wa 2015 uliofanyika jijini Johannesburg, pamoja na mambo kumi muhimu ya ushirikiano yaliyofikiwa kati ya China na Afrika, rais Xi pia aliahidi kuwa nchi yake itatoa jumla ya dola takribani bilioni 60 za Kimarekani kwa ajili ya mikopo na msaada kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo barani Afrika

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako